Saturday, May 3, 2014

Mfumo wa kielektroniki waongeza mapato Manispaa ya Kinondoni




Ofisa Uhusiano wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Bw. Sebastian Mhowera akieleza kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mfumo mpya wa kielektroniki wa ukusanyaji  mapato unatumiwa na manispaa hiyo,wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari(MAELEZO) Fatma Salum. 



Mchambuzi wa Mifumo ya Komputa Bw. Jackson Kiema akiwaonyesha waandishi wa habari(hawapo pichani) mashine ya kielektroniki inayotumika katika ukusanyaji wa mapato na kuhifadhi taarifa za mapato, wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Afisa Uhusiano wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Bw. Sebastian Mhowera. 

(Picha zote na Hassan Silayo-MAELEZO)
  
MFUMO MPYA WA UKUSANYAJI WA MAPATO 
Kutokana na kukua kwa sekta ya mawasiliano nchini, Manispaa ya Kinondoni imeanzisha utaratibu wa ulipaji wa kodi kwa kutumia huduma ya simu za mkononi na Max-malipo.
Huduma hiyo mpya inayotolewa kupitia mfumo unaojulikana kama “e–payment system”,humwezesha mwananchi kulipa kodi yake muda wowote, kwa haraka na urahisi na mahali popote.
Huduma hii inatolewa na Manispaa kwa kushirikiana na wakala anayetambulika kama “Max-malipo” ambaye kupitia huduma zake mitaa 171 iliyopo katika Kata 34 imeunganishwa katika mifumo hiyo ya ulipaji kodi.
Mfumo huu wa ukusanyaji wa kodi ndani ya Manispaa ni hatua ya utekelezaji unaozingatia maelekezo ya waraka wa Serikali Na. 5 wa mwaka 2009 unaohamasisha matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa lengo la kurahisisha utoaji wa huduma kwa Umma, kwa ufanisi na kwa wakati.
Kimsingi hatua hii inahamasisha ushirikishwaji wa wananchi katika utoaji wa maamuzi yanayohusu mambo yao na kuwezesha uwepo wa Serikali iliyo wazi, inayowajibika na makini katika kutekeleza majukumu yake kwa Taifa.
Hivyo basi kutokana na malengo na umuhimu wa kuwarahisishia wananchi, Manispaa iliona ni vema ikaingia haraka ndani ya utaratibu huu ili Mwananchi aweze kulipia kodi popote kwa kutumiaMax-malipo au wakala wa simu za mkononi yaani Tigo pesa Na.212888 na M-Pesa Na. 212888.

MAFANIKIO YALIYOPATIKANA.

Katika kipindi kifupi cha muda wa miezi 3, tangu mfumo huu mpya ulipoanzishwa rasmi kumekuwa na mafanikio makubwa kama ifuatavyo:-

·        Mapato yameongezeka kwa kiwango kikubwa mfano; ada ya kuchangia huduma za Afya (Cost sharing) imeongezeka kutoka Tshs. 45,000,000/= kwa wiki hadi kufikia Tshs. 65,000,000/= kwa wiki, sawa na ongezeko LA 69%

·        Chanzo cha kodi ya majengo hadi mwishoni mwa Machi tulikusanyaTshs. 339,000,000/= tofauti na awali ambapo hadi kipindi kama mwaka 2013 tulikusanya sawa na ongezeko la asilimia 269 hiki Tshs. 126,000,000/=

·        Maeneo mengine ongezeko la mapato limezidi bajeti ya mwaka iliyotakiwa kukusanywa. Kwa mfano katika ushuru wa huduma za jiji (City Service Kavy) ambapo tumezidi kwa 18%

·        Ushuru wa Masoko umeongezeka kwa wastani wa asilimia 20 ya lengo la kila mwezi.

·        Lesseni za biashara hadi Machi tumekusanya Tshs. 2.4 Bilioni sawa na 93% ya bajeti ya Manispaa ya chanzo hiki ya Tshs. 2.6 Bilioni kwa mwaka.

Napenda kuwahakikishia wananchi wa Kinondoni kuwa Manispaa ya Kinondoni itazidi kuboresha huduma zake ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa na kuwawezesha kuwa na maisha bora kutokana na mafanikio haya, lipa.

Lipa kodi kwa maendeleo ya Manispaa yako.
IMETOLEWA NA

SEBASTIAN MODESTUS MHOWERA
AFISA UHUSIANO WA MANISPAA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI
SIMU NA: 0754-227024

No comments:

Post a Comment