Monday, May 5, 2014

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja afanya ziara Wialaya ya Kahama


Moja kati ya mabango ambayo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja, alikutana nayo alipofika katika kijiji cha Isaka, wilayani Kahama wakati wa ziara yake.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja (wa pili kulia), akiwa amembatana na Wabunge wa Jimbo la Msalala, wilayani Kahama, Ezekiel Maige pamoja na Suleiman Nchambi wa Kishapu wakiwasili katika Kijiji cha Isaka wilayani Kahama kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa ilani ya chama hicho leo, ikiwa ni pamoja kukabidhi mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati katika kijiji hicho.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja (kulia), akiwa ameshikilia birika ikiwa ni miongoni mwa vitendea kazi vilivyokabidhiwa na Mbunge wa Kishapu, Suleiman Nchambi (katikati) kwa Kijiwe maarufu cha Kahawa kiitwacho BBC. Kushoto ni Mwenyekiti wa Shina la Wakereketwa wa kijiwehicho, katika Kata ya Isaka, wilayani Kahama, Ally Salum Msangi.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja (katikati), Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige (kulia) na Mbunge wa Kishapu, Suleiman Nchambi, wakinywa kahawa inayopikwa katika kijiwe cha BBC katika Kijiji cha Isaka Kata ya Isaka, wilayani Kahama leo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja (kulia), akikabidhi mifuko ya saruji 10 kutoka Ofisi ya chama hicho Mkoa kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Isaka, Said Hamad Shanduti (aliyevaa kofia kushoto) kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya kijiji hicho.

No comments:

Post a Comment