*Aupigia debe muziki wa injili
Mbunge wa Sengerema mkoani Geita, William Ngeleja akizindua albamu ya Msaada Wangu wa Karibu ya Msanii Grace Mwikabwe wakati wa Tamasha la Injili kwenye uwanja wa CCM Kirumba. Wa kwanza kushoto ni Grace Mwikwabe na kulia ni Alex Msama.
Maaskofu, Wachungaji na mgeni rasmi, Mbunge William Ngeleja, wakishikilia albam ya Msaada Wangu wa Karibu kwa ajili ya kuiombea kabla ya kuznduliwa jana.
William Ngeleja akihutubia mamia ya watazamaji wa tamasha la muziki wa injlili.
Watazamaji wakifuatilia tamasha hilo.
Rose Mhando akiwarusha waatazamaji.
Watazamaji wakiwa katika tamasha hilo pamoja na familia zao.
Na Mwandishi wetu
MBUNGE wa Bunge Maalum la Katiba,William Ngeleja, ameupigia debe Muziki wa Injili kuwa unayofasi ya kubwa ya kuhubiri amani nchini mbali ya kuhubiri jamii kumtukuza na kumcha Mungu.
Alisema amani iliyopo nchini imejengwa na watu wengi wakiwemo wasanii wa nyimbo za injili,Maaskofu,Wachungaji na watu wengine wengi hivyo kwa pamoja tutazidi kuimarisha nchi yetu.
Alitoa kauli hiyo jana Jijini Mwanza kwenye uwanja wa CCM Kirumba, kabla ya kuzindua albamu ya Msaada Wangu wa Karibu ya msanii Grace Mwikwabe
“Alichofanya hapa msanii huyo ni mchango mkubwa kwa amani ya Tanzania ambayo imejengwa na watu wengi.Hivyo Muziki huu unayo nafasi kubwa ya kuhubiri amani hiyo,”alisema Ngeleja
Hata hivyo Waziri huyo wa zamani wa serikali ya awamu ya nne,aliwashuruku Viongozi wa Kiroho kwa ushiriki wao wa kukubali mpango wa Mungu,Mwanza kuwa eneo la kuhubiri amani, neno la Mungu na nyimbo za kumhubiri Mungu,kwamba ni jambo jema kumwimbia Bwana.
Akizungumzia mchakato wa katiba alisema wabunge hao wamelitia taifa aibu kubwa,kwa sababu ya njia kutokuwa nyeupe wala nyoofu na akadai hakuna mafanikio bila kuwa na changamoto.
Alisema minyukano ndani ya Bunge hilo la Katiba,isiwakatishe tamaa,lakini kwa maombi ya Viongozi wa dini,mchakato huo utafika salama na hatimaye kujenga mazingira mazuri ya Watanzania kuwa na Katiba nzuri.
“Sisi kama taifa katika kipindi hiki kigumu cha kupatia utaratibu wa kuongoza nchi yetu,na utaratibu wa injili kuhubiriwa na amani kuwepo.Bunge la Katiba tumelitia aibu kubwa taifa lakini hakuna mafanikio bila kupitia changamoto mbalimbali,”alisema Ngeleja
No comments:
Post a Comment