Thursday, May 15, 2014

POLISI JIJINI DAR ES SALAAM WAFUMUA MTANDAO WA MAKOSA YA UVUNJAJI KWA KUKAMATA MAJAMBAZI SUGU 15 NA VITU MBALIMBALI.


Jeshi la Polisi Kanda Maalum kwa kutumia kikosi maalum cha Kiintelijensia (special intelligence task force) limefanikiwa kuufumua mtandao unaojihusisha na ujambazi jijini Dar es Salaam ikiwemo kuhusika na uvunjaji na kisha kupora mali mbalimbali zikiwemo nyumba za ibada.

Katika oparesheni hiyo iliyoanza tarehe 29/04/2014, wamekamatwa majambazi sugu wawili ambao baada ya kuhojiwa waliwataja wenzao wengine kumi na tatu (13) wanaoshirikiana nao katika matukio ya ujambazi na kufanya idadi yao kufikia kumi na tano.

Watuhumiwa waliokamatwa na kutaja mtandao mzima ni SHABAN S/O MAFURU, Miaka 36, Mkazi wa Magomeni na ABDALLAH S/O HUSSEIN, Miaka 52, Mkazi wa Tabata Mawenzi, ambao wote walikutwa kwenye gari namba T259 ADB, T/RAV rangi ya Silver wakiwa wamepakia vitu mbalimbali vya wizi kama ifuatavyo:

·         Moving Camera - 4.
·         Stand mbili za Moving Camera.
·         Desk-top computer – 2
·         Deki mbili za DVD.

Inasemekana mali hizi walizokutwa nazo watuhumiwa hawa ziliibwa katika ofisi za ISLAM INTERNATIONA LTD zilizopo maeneo ya mabibo jijini Dar es Salaam.
Baada ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumi na tano walihojiwa na kukiri kuhusika katika matukio kadhaa ya uvunjaji na uporaji kama ifuatavyo:

·         Tukio la tarehe 01/05/2014 maeneo ya REGENT ESTATE katika ofisi za NAIRO ambapo walivunja na kuiba viyoyozi (Air Condition) 120 na vitu vingine.

·         Tarehe 22/04/2014 huko maeneo ya Mwenge katika duka SAMSUNG, walivunja na kuiba TV Set zipatazo nane (8) na simu za mkononi mbalimbali.

·         Tarehe 17/04/2014 maeneo ya MASAKI walivunja Supermarket iitwayo SHIREJEES na kupora fedha TSh. 19,000,000/= (Millioni kumi na tisa), Monitor mbili za Computer, LCD TV Set mbili, na pombe kali za aina mbalimbali.

·         Pia wamekiri kuvunja Makanisa mawili moja ni lile la K.K.K.T Usharika wa Magomeni na kupora pesa taslim Tsh. 8,000,000/=. Kanisa lingine walilokiri kuvunja ni lile la AICT ambapo walipora Tsh 500,000/=, Desk-top Computer mbili aina ya DELL, Laptop mbili aina ya DELL, na Projctor moja aina ya Sony.

·         Wamekiri kuhusika katika uvunjaji kwenye ofisi za Shule ya Sekondari ya LOYOLA iliyoko Mabibo na kuiba DOLLA ZA KIMAREKANI zipatazo 8000 na Shillingi za Kitanzania 9,000,000/=

Watuhumiwa wengine waliokamatwa wanaounda mtandao huu ni kama ifuatavyo:
·         FLORIAN S/O PHILOMON @ K.K, Miaka 35, Mkazi wa Manzese.
·         MATOKE S/O MAGERE, Miaka 30, Mkazi wa Kigogo Kintinku.
·         RASHID S/O MUSSA @ GAIDI, Miaka 42, Mkazi wa Kariakoo Mchikichini.
·         ATHUMAN S/O SALEHE @ KIDINYU, Miaka 30, Mkazi wa Magomeni Makuti.
·         AZIZI  S/O SAID FADARI, Miaka 38, Mkazi wa Kiwalani Minazi Mirefu
·         IBRAHIMU S/O KINGU, Miaka 50, Mkazi wa Temeke Mikoroshini.
·         THOMAS S/O KIMAMBI, Miaka 33, Mkazi wa Ubungo External.
·         JOSEPH S/O JOSEPH THOMAS, Miaka 32, Mkazi wa Kimara Stop Over.
·         STEPHANO S/O SAMWEL @ LIKONGO, Miaka 37, Mkazi wa Mburahati Mianzini.
·         NICKO S/O NUSULUPIA HAULE @ NICK BUTY, Miaka 31, Mkazi wa Mburahati Mianzini.
·         KUDRA S/O MOHAMED, Miaka 30, Mkazi wa Ubungo.
·         HAMISI S/O SALUM SALEHE, Miaka 31, Mkazi wa Kimara Rombo.
·         MOHAMED S/O RASHID, Miaka 30, Mkazi wa Kimara Rombo.


No comments:

Post a Comment