Sunday, June 8, 2014

Mahafali ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu Dodoma, walio wanachama wa CCM yafana

*Waziri Prof. Mwandosya awa mgeni rasmi
*Awataka wasomi kujiajiri badala ya kutegemea vyeti
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Dodoma Mjini, Kanuti Ndaghine akimkabidhi mmoja wa wanafunzi wanaochukua Diploma katika Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP), Ruth Matoke kadi ya kujiunga na chama hicho, ambapo jumla ya wanachama wapya 230, walipokea kadi kabla ya kuelekea kwenye mahafali yaliyowaunganisha wanafunzi wa Vyuo vyote vilivyopo mkoani Dodoma. 
Waziri asiye na Wizara Maalum, Profesa Mark Mwandosya akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na wanafunzi 1500 wa Vyuo vyote, vilivyopo mkoani Dodoma ambao pia ni wanachama wa CCM waliojumuika kwenye mahafali ya pamoja kabla ya mitihani inayotarajia kuanza wiki hii inayoanza.
Wanafunzi wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP), wakipokea kiapo cha utii mara baada ya kupokea kadi za uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kabla ya mahafali yaliyowakutanisha wanafunzi wa Vyuo vyote, ambao ni wana CCM.
Mjumbe wa Halimashauri Kuu ya Taifa (NEC), Mkoa wa Dodoma Anthony Mavunde akimshukuru Waziri asitye na Wizara Maalum, Profesa Mwandosya kwa kushiriki katika mahafali hayo.
Waziri asiye na Wizara Maalum, Prof. Mark Mwandosya (katikati), akimpongeza mwanafunzi wa mwaka wa Tatu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Razao Noemio Jose, kutoka Msumbiji, ambaye anashirikiana vizuri na wana CCM, waliopo ndani ya chuo hicho, wakati wa mahafali ya umoja wa wanafunzi wa CCM, waliopo vyuoni Dodoma. Kushoto ni Mwenyekiti wa maandalizi, Donald Haule.
Wanafunzi wa Vyuo vilivyopo mkoani Dodoma, ambao pia ni wana CCM, wakiwa katika ukumbi wa Loyal, wakati mahafali yao. (Picha zote na John Banda)

Na John Banda, Dodoma
WASOMI wengi nchini wameshindwa kujiajiri kutokana na kutojua kuwa Elimu waliyonayo imewafungua akili ili waweze kufanya mambo yao, wakiwa na uelewa mzuri, hali inayowafanya kutegemea vyeti walivyonavyo.


Kauli hiyo, ilitolewa na Waziri Ofisi ya Rais asiyekuwa na Wizara
Maalum, Profesa Mark Mwandosya, alipokuwa kwenye mahafali ya wanafunzi ambao ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wa Vyuo Vikuu vilivyopo mkoani Dodoma.


Mwandosya alisema wengi wamejikuta wamekwama kujiajiri kutokana na kusubiri ajira bila kujua kuwa elimu waliyopata zinaweza kuwasaidia kufanya mambo ya kimaisha katika uelewa walioupata vyuoni na vinginevyo.


Alisema hivi sasa ushindani katika soko la ajira ni mkubwa kutokana na wasomi kuwa wengi tofauti na kipindi yeye alichopata Phd ambapo yeye kama siyo wa kwanza basi alikuwa wa pili hivyo ni afadhali wakaweka malengo ya kujiari pindi wanapomaliza masomo yao.


Alitoa mfano kwa Waafrika Mashariki, wengi wanaofanya kazi katika mahotel nchini Dubai kuwa ni Wakenya, Uganda, Rwanda na Burundi, ambao pamoja na kuwa na shahada za uzamili wanaamua kufanya kazi hata ambazo hawakutegemea kutokana na kukosa ajira.


‘’Vijana wangu, najua mnaanza mitihani yenu wiki hii inayoanza,
hakikisheni mnajiwekea malengo ya kujiajiri pindi muondokapo vyuoni maana  kukosa malengo kutawafanya kutojituma na kujikuta kila siku mkiuza vyeti ambavyo kila mtu anavyo badala ya ubora wa elimu milioupata vyuoni’’, alisema.


Aliongeza kuwa ni vizuri kuwa wabunifu na kujituma katika kila
watakachofanya bila kujali hadhi ya vyeti walivyonavyo.


Awali Chama cha CCM kilipokea jumla ya wanachama wapya 230 na kuwakabidhi kadi wasomi wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijiji (IRDP) na wengine sita waliokabadhi kadi wakitokea Chadema, akiwemo kiongozi wao, Belina Maingu maarufu kwa jina la Baozi.


Jumla ya Wanafunzi 1500 wa vyuo 10, vilivyopo mokoani Dodoma, ambao ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walikutana kwenye mahafali ya kwanza yaliyowakutanisha kwa pamoja mwaka huu tofauti na miaka mingine ambayo kila chuo hufanya mahafali yake chenyewe.

No comments:

Post a Comment