Washindi
wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kutoka Kanda ya Ziwa
wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere, Jijini Dar es Salaam
jana kwaajili ya Kuingia kambini tayari kwa safari ya kushindania
Milioni 50 katika fainali itakayofanyika mwishoni mwa Mwezi wa Nane.
Washindi
wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kanda ya Nyanda za Kusini,
Stephen Mapunda(mwenye kofia nyekundu) na Mtawa Kaparata (mwenye fimbo)
wakiwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere jana tayari kwa safari
ya kushindania Shilingi Milioni 50 za Kitanzania
Washindi
wa Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini wakibadilishana Mawazo wakati
walipowasili katika uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere, Jijini Dar Es Salaam
jana.
Washindi
wa Tanzania Movie Talents (TMT) wakielekea kwenye basi la TMT tayari
kwa kupelekwa kwenye Hoteli kwaajili ya Kupumzika mara baada ya kuwasili
katika Uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere, Jijini Dar Es Salaam. (Picha
zote na Josephat Lukaza)
No comments:
Post a Comment