Balozi Joseph Edward Sokoine akila kiapo mbele ya Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete leo amemwapisha Balozi mmoja pamoja na wajumbe
wanne wa Tume ya Operesheni Tokomeza katika hafla fupi iliyofanyika
Ikulu, jijini Dar es Salaam leo mchana. Balozi aliyeapishwa ni
Joseph Edward Sokoine ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika
katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Wajumbe
walioapishwa ni pamoja na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji mstaafu Hamisi
Amiri Msumi, Jaji mstaafu Steven Ernest Ihema, Jaji mstaafu Vincent
Damian Lyimo pamoja na katibu wa tume hiyo Bwana Frederick Kapela.
Balozi Joseph Edward Sokoine akupokea miongozo ya kazi na kupongezwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
Balozi Joseph Edward Sokoine akipongezwa na Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Wajumbe
wa Tume ya operesheni Tokomeza wakiwakatika picha ya pamoja na Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal (wanne
kushoto) na Katibu Mkuu Kiongozi. Balozi Ombeni Sefue (Wapili kulia),
wajumbe hao kutoka kushoto ni Katibu wa Tume hiyo, Bw. Frederick Kapela
Manyanda, Jaji mstaafu Vincent Damian Lyimo (wapili kushoto), Jaji
mstaafu Hamisi Amiri Msumi (watatu kushoto), na Jaji Mstaafu Steven
Ernest Ihema(kulia),Wasita kushoto ni Balozi Joseph Edward Sokoine.
(Picha zote na Freddy Maro)
No comments:
Post a Comment