Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa akimtunuku
Cheti mmoja wa Wahitimu wa Mafunzo
ya Kuwajengea Uwezo Maafisa Elimu Vifaa na Takwimu (SLOs) na Maafisa Elimu
Taaluma (DAOs) (Msingi Na Sekondari) Tanzania Bara Kuhusu Kukabiliana na
Majanga Katika Taasisi za Elimu;
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, Mwishoni mwa Wiki amefunga Mafunzo
ya Kuwajengea Uwezo Maafisa Elimu Vifaa na Takwimu (SLOs) na Maafisa Elimu
Taaluma (DAOs) (Msingi Na Sekondari) Tanzania Bara Kuhusu Kukabiliana na
Majanga Katika Taasisi za Elimu, Yaliyofanyika ADEM - Bagamoyo Kuanzia tarehe
19/05/2014 hadi 06/06/2014.
Mafunzo haya yalishirikisha jumla ya Maafisa Elimu
Vifaa na Takwimu na Maafisa Elimu Taaluma (Msingi na Sekondari) wapatao 636
kutoka Tanzania Bara. Maafisa hawa wanahusika moja kwa moja katika kusimamia
utekelezaji wa utoaji Elimu bora nchini katika ngazi ya halmashauri chini ya
mkakati mpya wa Matokeo Makubwa Sasa (Big
Results Now) katika sekta ya elimu.
Mafunzo haya yatawawezesha kusimamia utoaji wa elimu
bora shuleni na pia kutumia mbinu mbalimbali walizojifunza katika kuzuia na
kukabiliana na majanga yanapotokea katika maeneo yao. Maafisa hao wataweza
kutoa elimu kuhusu majanga kwa walimu, wanafunzi, viongozi na wadau wote wa
elimu katika halmashauri zenu. Aidha, Elimu waliyoipata itawawezesha pia kuwa
na uwezo wa kusimamia, kufuatilia na kuimarisha miundombinu shuleni na kuchukua
hatua za tahadhari zitakayowezesha kukabiliana na majanga, mbalimbali kama vile
umuhimu wa milango ya majengo ya shule kufungukia nje, kuwa na vifaa vya kuzima
moto na kuwa na visanduku vya huduma ya kwanza.
Shule zetu zimekuwa zikikumbwa na majanga
mbalimbali kwa mfano moto, mafuriko na vimbunga. Majanga haya yameleta athari
kubwa kwa maisha ya walimu na wanafunzi, katika majengo yakiwemo madarasa,
nyumba za walimu, maabara na vyoo.
Samani za shule, vifaa vya kufundishia na kujifunzia, barabara, huduma
za maji na umeme, viwanja vya michezo na mazingira yote ya shule yamekuwa
yakiharibiwa na majanga. Imeshuhudiwa moto ukiteketeza shule za Sekondari za
Shauritanga, Idodi, Morogoro n.k na kusababisha vifo kwa wanafunzi na
kuharibika kwa miundo mbinu ya shule. Pia tumeshuhudia mafuriko yakisababisha
kutoendelea kwa masomo katika Wilaya za Kilosa, Kyela, Ilala, Mvomero n.k
mafuriko haya yalisababisha shughuli za shule kukwama.
Serikali inaamini kuwa baada ya mafunzo haya, washiriki wataweza
kutimiza majukumu haya mapya kama ifuatavyo:
·
kuunda Kamati za kukabiliana na Majanga Shuleni;
·
kuandaa mipango kazi ya kukabiliana na majanga katika
ngazi ya halmashauri na shule;
·
kuboresha miundombinu ya shule ikiwemo milango
kufungikia nje, kuweka vizima moto (fire extinguishers), ndoo za michanga na
kuboresha mazingira ya shule;
·
kujenga uelewa wa pamoja wa namna ya kukabiliana na
majanga miongoni mwa walimu, wanafunzi na jumuiya inayozunguka shule
·
kujenga mtandao (network) wa kukabiliana na majanga
kati ya shule na jumuiya inayozunguka shule;
·
kufanya ufuatiliaji na tathmini kuhusu majanga
shuleni; na
kuandika
taarifa sahihi kuhusu uwezekano wa kutokea majanga na madhara ya majanga shuleni
mara yanapotokea.
Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa akitoa hotuba ya kufunga Mafunzo ya Kuwajengea Uwezo
Maafisa Elimu Vifaa na Takwimu (SLOs) na Maafisa Elimu Taaluma (DAOs) (Msingi
Na Sekondari) Tanzania Bara Kuhusu Kukabiliana na Majanga Katika Taasisi za
Elimu;
- Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa akimtunuku Cheti mmoja wa Wahitimu wa Mafunzo ya Kuwajengea Uwezo Maafisa Elimu
Vifaa na Takwimu (SLOs) na Maafisa Elimu Taaluma (DAOs) (Msingi Na Sekondari)
Tanzania Bara Kuhusu Kukabiliana na Majanga Katika Taasisi za Elimu;
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa akimtunuku Cheti mmoja wa Wahitimu wa Mafunzo ya Kuwajengea Uwezo Maafisa Elimu
Vifaa na Takwimu (SLOs) na Maafisa Elimu Taaluma (DAOs) (Msingi Na Sekondari)
Tanzania Bara Kuhusu Kukabiliana na Majanga Katika Taasisi za Elimu;
- Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (mwenye suti nyeusi katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na Wahitimu wa Mafunzo
ya Kuwajengea Uwezo Maafisa Elimu Vifaa na Takwimu (SLOs) na Maafisa Elimu
Taaluma (DAOs) (Msingi Na Sekondari) Tanzania Bara Kuhusu Kukabiliana na
Majanga Katika Taasisi za Elimu;
- Baadhi ya Wahitimu wa Mafunzo
ya Kuwajengea Uwezo Maafisa Elimu Vifaa na Takwimu (SLOs) na Maafisa Elimu
Taaluma (DAOs) (Msingi Na Sekondari) Tanzania Bara Kuhusu Kukabiliana na
Majanga Katika Taasisi za Elimu;
Baadhi ya Wahitimu wa Mafunzo ya Kuwajengea Uwezo Maafisa Elimu
Vifaa na Takwimu (SLOs) na Maafisa Elimu Taaluma (DAOs) (Msingi Na Sekondari)
Tanzania Bara Kuhusu Kukabiliana na Majanga Katika Taasisi za Elimu;
No comments:
Post a Comment