Thursday, July 31, 2014

Ebola: Liberia yaomba msaada



Waziri wa habari wa Liberia Lewis Brown amesema nchi yake haiwezi kuimudu hali ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola. Amesema Liberia inahitaji msaada toka jumuiya za kimataifa kutuma wataalam wa tiba ili wasaidie.
Brown ameuelezea mlipuko wa ugonjwa huo kuwa si wa kawaida.
“Huu bado ni mshituko. Uwezo wa huduma za afya ya jamii na vifaa vimezidiwa. Maambukizi na kutapakaa ni kwa namna ambayo hatukuwahi kuwa nayo. Tunapungukiwa wahudumu wa afya na kwakweli tunahitaji wataalam zaidi wa afya” alisema Brown
Amesema Liberia inahitaji vifaa vya huduma za kiafya, wataalam wenye uzoefu wa kiafya kutokana na hali ya ugonjwa huo ilivyo,tunahitaji chochote kinachoweza kutusaidia kupambana na ugonjwa wa Ebola amesisitiza
Serikali ya Uingereza imeitisha mkutano wa dharura kupanga hatua za kuchukuliwa kwa ushirikiano na serikali ya Ufaransa na Marekani. Umoja wa Ulaya imetenga dola milioni 2 nukta 5 za ziada ili kupambana na Ebola. Tangu Ebola ilipoanza mwezi Februari mwaka huu, zaidi ya watu 670 wamefariki huko Afrika Magharibi katika nchi ya Sierra Leone, Liberia, Guinea na Nigeria.

No comments:

Post a Comment