Thursday, July 24, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA 45 WA CPA JIJINI ARUSHA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wajumbe wa Chama cha Wabunge kutoka nchi za Jumuiya ya Madola (CPA) katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha. Mheshimiwa Makamu wa Rais alifungua mkutano wa 45 wa CPA unaozikutanisha nchi za Afrika unaofanyika nchini Tanzania kuanzia leo Julai 24 hadi Julai 27, 2014. Mkutano huo sambamba na masuala mengine pia unajadili juu ya wajibu wa mabunge na mchango wao katika kusimamia utawala bora pamoja na kusaidia serikali za Afrika kubuni mipango ya maendeleo inayolenga vizazi vya sasa kwa lengo la kuijenga Afrika ijayo
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Makamu wa Rais wa CPA na Spika wa Ufalme wa Lethoto, Enoch Sephir Motanyane,   wakati akiondoka nje ya ukumbi wa AICC baada ya kufungua rasmi mkutano wa 45 wa CPA unaozikutanisha nchi za Afrika unaofanyika nchini Tanzania, jijini Arusha kuanzia leo Julai 24 hadi Julai 27, 2014.
 Burudani ilikuwepo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wabunge baada ya kufungua rasmi mkutano wa 45 wa CPA unaozikutanisha nchi za Afrika unaofanyika nchini Tanzania, kuanzia leo Julai 24 hadi Julai 27, 2014.

No comments:

Post a Comment