Sehemu ya waalikwa waliofika katika maonyesho ya Biashara ya Eid el Fitri yanayoandaliwa kwa pamoja kati ya TANTRADE na Wizara ya Biashara ya Zanzibar kila mwaka wakimsikiliza mgeni Rasmi katika ufunguzi wa maonyesho hayo.
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui (kulia), akikata utepe kufungua maonesho ya Biashara ya Eid el Fitri katika viwanja vya Maisara Suleiman, mjini Zanzibar jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Sabetha Mwambenja na katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE, Anna Bulondo.
Waziri wa Biashara Viwana na Masoko Nassor Ahmed Mazrui akiangali bidhaa za wajasiriamali kwenye maonyesho ya Biashara ya Eid el Fitri katika kiwanja cha Maisara.
Waziri Mazrui akinunua bidhaa za wajasiriamali wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya Biashara ya Eid el Fitri katika kiwanja cha Maisara Mjini Zaznibar.
Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko wa Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui katika picha ya pomoja na viongozi mbali mbali. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar)
No comments:
Post a Comment