Friday, August 1, 2014

Israel yajiandaa tena kwa vita Gaza


Israel inasema kuwa Hamas ndio waliovunja makubaliano ya hivi karibuni ya kusitisha vita
Wanajeshi wa Israel wamewaonya raia wanaoishi katika ukanda wa Gaza, kusalia majumbani mwao huku wakijiandaa kuanza tena mashambulizi dhidi ya Hamas.
Hii ni baada ya makubaliano yaliyofikiwa ya kusitisha vita kwa masaa 72 kwa ajili ya kupitisha msaada wa kibinadamu kuvunjwa.
Taarifa kutoka kwa waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu imesema kuwa Hamas pamoja na makundi mengine aliyotaja kama ya kigaidi katika ukanda wa Gaza, yamekiuka makubalianyo hayo ya kusitisha vita.
Awali, maafisa wa Gaza walisema kuwa mashambulizi yaliyofanywa na Israel yaliwaua watu 4 katika eneo la Rafah Kusini mwa Gaza.
Maafisa wa Israel wamesema kuwa hatua hiyo ilikuwa kama jibu kwa shambulizi la roketi lililofanywa na Israel mpakani.
Hatua ya kuvunjwa kwa makubaliano ya kusitisha vita, saa chache kabla ya kuanza kutekelezwa, ilikuja licha ya shinikizo za kimataifa kwa pande hizo mbili kusitisha vita.
Usitishwaji wa vita angalu ulirejesha utulivu wa mda mfupi, katika eneo hilo ambalo limeshuhudia vita kwa mda mrefu.
Wapalestina 14 waliuawa usiku kucha kabla ya usitishwaji wa vita kuanza katika kile kilichosemekana kuwa mashambulizi mabaya kufanywa na israel hivi karibuni.
Wanajeshi 5 wa Israel waliuawa katika shambulizi lililofanywa na Wapiganaji wa Palestina.
Zaidi ya wapalestina 1400, wengi wakiwa raia , wameuawa katika mashambulizi hayo yanayofanywa na Israel. Ni waisraeli 63 pekee waliouawa.

No comments:

Post a Comment