Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linamshikilia
mlamavu aitwaye SAID S/O TINDWA, MIAKA 36, MKAZI WA VIJIBWENI
Wilaya ya Temeke kwa kosa la kufanya biashara ya dawa za kulevya.
Tarifa
za kiintelijensia zilizopatikana kupitia kwa raia wema ziliwafikia makachero
wa Polisi kuwa mlemavu huyo ambaye mguu wake wa kulia ni wa bandia amekuwa
akiutumia vibaya mguu huo kwa kuficha dawa za kulevya ambazo aliwauzia
watumiaji. Aidha kila kete alikuwa akiuza kwa shilingi Tsh.1000.
Ilikuwa mnamo tarehe 01/08/2014 katika mtego maalumu uliowekwa na
askari wa upelelezi ndipo mlemavu huyo alikamatwa akiuza dawa hizo kwa
wateja wake baada ya kuzitoa alikozificha ambapo ni ndani ya mguu huo
wa bandia.
Uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba mtuhumiwa huyo amekuwa
akitumia mbinu hiyo kwa muda mrefu kabla ya kukamatwa. Aina ya dawa
alizokuwa akiuza ni zile za viwandani kama vile Cocein , Heroin na wakati
mwingine bhangi. Uchunguzi wa shauri hili bado unaendelea na jalada
la kesi yake litapelekwa kwa mwanasheria wa serikali ili sheria iweze
kuchukua mkondo wake.
Aidha natoa onyo kwa watu wenye ulemavu kwamba wasitumie kigezo cha
ulemavu kufanya uhalifu kwa makusudi kwani wanawaharibia walemavu wengine
ambao ni raia wema na ambao mara nyingi huonewa huruma na kutotiliwa
mashaka.
S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment