Jeshi la Polisi Kanda Maalum DSM linawashikilia wanawake watatu kwa
kosa la kujihusisha na mtandao haramu wa nyara za Serikali. Mnamo tarehe
23/07/2014 huko eneo la Mbagala Mission Polisi walipata taarifa kutoka
kwa msiri kuwa eneo hilo lina watu wanajihusisha na biashara ya nyara
za serikali.
Polisi walifika eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata WEMAEL
D/O MSHANA na alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa na vipande sita
vya meno ya tembo vyenye thamani ya dola za Kimarekani 30,000 (Dolla
elfu thelathini) sawa na shilingi za kitanzania 49,750,000/= (milioni
arobaini na tisa mia saba hamsini elfu) ambao ni sawa na tembo wawili
waliouawa.
Taarifa za awali zinaonyesha kuwa mtuhumiwa anashirikiana na watuhumiwa
wengine ambao ni UPENDO D/O MSHANA, Miaka 33, na STELLA D/O DANIEL,
Miaka 17, Mwanafunzi wa Chuo cha Genessis cha Mtoni kwa Azizi Ali ambao
nao wamekamatwa.
Uchunguzi zaidi unafanyika kwa kushirikiana na Idara ya wanyama pori
ili kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake.
S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment