Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linamshikilia mtu mmoja
VENANCE S/O MANYIKA, Miaka 38, Mkazi wa Mbagala Massion kwa kosa la
kukutwa na ngozi ya chui kinyume cha sheria.
Mtuhumiwa huyu alikamatwa
tarehe 29/07/2014 huko Mbagala Mission na askari waliokuwa katika misako
inayoendelea yenye lengo la kupambana na uhalifu jijini Dar es Salaam.
Wakiwa katika misako hiyo Polisi walipokea taarifa kuwa kuna mtu wanayemuhisi
kujihusisha na uuzaji wa nyara za Serikali ndipo walipofika eneo la
tukio na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa.
Upelelezi wa shauri hili unaendelea
na jalada la mtuhumiwa litapelekwa kwa mwanasheria wa Serikali ili sheria
iweze kuchukua mkondo wake.
S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment