Monday, September 5, 2016

DKT INTERNATIONAL TANZANIA YAZINDUA ‘TRUST COMMUNITY MATERNITY HOMES

 Meneja Masoko wa DKT international Tanzania Sialouise Shayo akizungumza na wageni mbalimbali waliofika kujionea Kliniki mpya na ya kisasa iliyozinduliwa katika makao makuu ya Shirika hilo hivi karibuni Masaki, jijini Dar es salaam kwa ajili ya Afya ya uzazi kwa kina mama.
 Meneja Mradi wa programu ya Trust community maternity homes kutoka DKT International Tanzania Carol Francis Mango akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa kliniki hizo mpya zilizotengenezwa maalumu kwaajili ya kukidhi mahitaji ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa wanawake wanaoishi kwenye miji midogo katika jamii yetu. Uzinduzi wa kliniki hizo ulifanyika jana katika makao makuu ya Shirika hilo jijini Dar es salaam.
 Mkunga kutoka DKT International Tanzania Adella Hugo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na huduma mbalimbali zinazopatikana kwenye Kliniki mpya ya uzazi wa Mpango iliyozinduliwa jana katika Makao makuu ya Shirika hilo Masaki, jijini Dar es salaam. Kliniki hiyo ni maalumu kwaajili ya kukidhi mahitaji ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la DKT International Tanzania Raphael da Silva akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kliniki mpya za Shirika hilo zijulikanazo kama “Trust community maternity homes”. Kliniki hizo mpya ni maalumu kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa wanawake wanaoishi kwenye miji midogo katika jamii yetu. Uzinduzi huo ulifanyika jana katika Makao makuu ya Shirika hilo Masaki, jijini Dar es salaam.
Meneja Masoko wa DKT International Tanzania Sialouise Shayo akionyesha baadhi ya bidhaa kwa waandishi wa habari zinazopatikana kwenye Kliniki mpya ya uzazi wa Mpango iliyozinduliwa jana katika Makao makuu ya Shirika hilo Masaki, jijini Dar es salaam. Kliniki hiyo ni maalumu kwaajili ya kukidhi mahitaji ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango.

SHIRIKA lisilo la kiserikali la DKT International Tanzania limezindua mfano wa Kliniki mpya ziitwazo “Trust community maternity homes kwa ajili ya wananchi wa kipato cha kawaida zinazoendeshwa na wakunga mbalimbali.

“Trust Community Maternity Homes” – Ni kliniki zinazojitosheleza zilizotengenezwa kwa ubunifu kwa kutumia kontena ya kusafirishia mizigo, kliniki hizi zimetengenezwa maalumu kwaajili ya kukidhi mahitaji ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa wanawake wanaoishi kwenye miji midogo katika jamii yetu.

Kiliniki za “Trust Community Maternity Homes”  zilizinduliwa kwa umma  wakati wa uzinduzi wa kliniki ya “Trust Health & Wellness Clinic “ ya Dar Es Salaam na ofisi  mpya za DKT International Tanzania  mnamo tarehe mbili September, 2016

“Kila mwaka, wanawake milioni moja hapa Tanzania ambao hawakukusudia kupata ujauzito hupata ujauzito” alisema mkurugenzi mkuu wa DKT international, Raphael da Silva.

“Hali hii si tu kuwa ina athiri wanawake hawa kifedha, afya zao binafsi na hali ya kiuchumi ya familia zao, lakini pia zinapelekea kuongeza uhitaji wa Serikali kutoa huduma za kiafya pamoja na elimu kwa watoto hawa .Kama tunaweza kufanikisha kutoa huduma zenye ubora wa hali ya juu za afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa jamii katika miji midogo na wanajamii ambao hawapati huduma hizi kiurahisi, tutafanikiwa kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya wanawake hawa” alisema.

“Trust Community Maternity Homes ni kliniki zinazojitosheleza ndani ya kontena la kusafirishia mizigo, zinazoendeshwa na wakunga wataalamu na wenye uzoefu wa muda mrefu kama washirika chini ya kliniki mama za “Trust health and wellness clinics” .  Alisema meneja mradi, Karoli Mango.

“Kliniki hizi zinatoa ubora ule ule wa huduma , usiri na msaada  sawa sawa na Kliniki zetu nyingine za Trust  zinazopatikana mikoani hapa nchini .Kliniki yetu ya kwanza ya “ Trust community maternity homes” ya mjini  Kahama iko katika hatua za mwisho za  maandalizi kabla ya ufunguzi” aliongeza.

Trust ina mpango wa kuingia mikataba yenye masharti mepesi na wakunga wazoefu ambayo itawawezesha kukodisha na baadae kuzi miliki kliniki hizi.  Wakunga wanaotoa huduma hizi watatumia kliniki hizi ambazo ziko ndani ya kontena ambazo zinatumia umeme wa sola , zenye uwezo wa kutoa huduma kamili za afya ya uzazi na uzazi wa mpango, pamoja na huduma nyingine za afya kwa jamii. Wakunga hawa watajipatia kipato kwa kutoza kiasi kidogo cha fedha kwa huduma na bidhaa zitakazo tolewa katika kliniki hizi. 

Kwa sasa , kuna “ Trust health and wellness  clinic” nne  ambazo ziko Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya and Mwanza  na pia kuna kliniki  na hospitali washirika  30  ambazo zinatoa huduma kwa kutumia chapa ya Trust. 

Kliniki ya Msasani peninsula ya Dar Es Salaam ilifunguliwa mapema mwezi Julai.

No comments:

Post a Comment