Thursday, September 29, 2016

Majaliwa atoa mwezi watumishi wahamie Kibiti




WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewapa mwezi mmoja watumishi wa umma ambao hawajaripoti kwenye kituo chao cha kazi katika Wilaya mpya ya Kibiti, mkoani Pwani kufika mara moja na kuanza kazi.
Agizo hilo alilitoa jana wilayani Kibiti akiwa kwenye ziara yake mkoani Pwani kukagua shughuli za maendeleo, utekelezaji wake na kueleza msimamo wa serikali kwa watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla.
Kabla ya kutoa agizo hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, Alvera Ndabagoye alimwambia Waziri Mkuu kuwa hadi sasa wilaya hiyo ina watumishi nane walioripoti kati ya watumishi 74.
"Mheshimiwa Waziri Mkuu, baada ya wilaya ya Rufiji kugawanywa na kuzaliwa wilaya mpya ya Kibiti watumishi pia waligawanywa na wengine TAMISEMI inatuletea, lakini hadi sasa nina watumishi nane, kati yao wakuu wa idara ni wawili," alisema Ndabagoye.
Amewataja watumishi hao kuwa ni Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mkuu wa Idara ya Uhasibu, wahasibu wawili, madereva wawili, Katibu Muhtasi na Ofisa Utumishi.
Amesema kati ya watumishi hao, sita wametokana na mgawanyo wa wilaya na wawili wametoka TAMISEMI. Kufuatia taarifa hiyo,Waziri Majaliwa alisema watumishi wote waliopangwa kufanya kazi katika wilaya hiyo,wanapaswa kuwepo ndani ya eneo hilo na kuwatumikia wananchi na kama kuna changamoto zinapaswa kushughulikiwa wakiwa kazini.
Waziri Mkuu," amesema."Natoa mwezi mmoja watumishi wote wanaopaswa kuwa hapa Kibiti,wafike pamoja na upya wenu, ingekuwa sio upya ningewapa muda mfupi zaidi
Amefafanua zaidi, kwa kusema changamoto za ukosefu wa nyumba za kuishi ni mambo yanayoweza kutafutiwa ufumbuzi wakati watumishi hao wakiwa kwenye eneo la kazi na kuwataka uongozi wa wilaya hiyo kuzungumza na Mifuko ya Hifadhi za Jamii na kuingia nao mikataba kuona jinsi watakavyojenga nyumba za makazi.
Amesisitiza Waziri Mkuu.kwa kusema waZungumzeni na mifuko ya hifadhi ije kuwajengea nyumba, ingieni mikataba nao, ni marufuku mtumishi wa Kibiti kuishi nje ya eneo lake la kazi,"
Akizungumzia majengo ya ofisi ya wilaya hiyo, Mkurugenzi Ndabagoye alisema kuna uhaba wa majengo ya ofisi wilayani Kibiti kutokana na upya wa wilaya hiyo lakini pamoja na hali hiyo yeye na watumishi hao wachache wamesharipoti kazini na kuanza kazi.
Ndabagoye. amesema"Mheshimiwa Waziri Mkuu pamoja na wilaya kuwa mpya, upungufu wa majengo na samani ni mkubwa, ila kwa vile tumedhamiria kuwatumikia wananchi tuko kwenye vituo vyetu vya kazi tunajua hizi ni changamoto tutazitatua ",
Awali akizungumza na watumishi wa wilaya hiyo,Waziri Mkuu aliwataka watumishi hao kutumia nafasi zao kwa manufaa ya nchi kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuibadilisha wilaya hiyo.
Akisoma taarifa ya wilaya hiyo kwa Waziri Mkuu, Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Gulamhussein Kifu alisema pamoja na mafanikio yaliyopo bado kuna changamoto zikiwemo migogoro ya wakulima na wafugaji,uvuvi haramu, miundombinu na uhaba wa watumishi.
Akijibu hoja mbalimbali, Waziri Mkuu alisema ni kweli maeneo mengi kuna uhaba wa watumishi wa kada mbalimbali na kusema ajira za watumishi hao zitatangazwa baada ya kukamilika kwa kazi ya uhakiki wa watumishi hewa, linaloendelea nchini kote.

No comments:

Post a Comment