Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilino Prof Makame Mbarawa
ameteuai wajumbe sita wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania.
Hatua hiyo inafuatia Rais Dk John Magufuli kumteua Luteni Kanali
Mstaafu, Haroun Ramadhan Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya ya Shirika la Posta
Tanzania hivi karibuni.
Taarifa ya Katibu Mkuu Wizara hiyo
anayeshughulikia Mawasiliano, Prof Faustine Kamuzora imesema Prof Mbarawa
ametangaza uteuzi huo leo kwa mujibu wa sheria za shirika la Posta Tanzania No
19 ya mwaka 1993 kifungu cha 1(b) na uteuzi huo ulianza tangu Septemba 5 mwaka
huu.
Wajumbe walioteuliwa kusaidiana na Luteni
Kanali Mstaafu Kondo na watadumu katika nyadhifa hizo kwa kipindi cha miaka
mitatu ni pamoja na Mhadhiri wa sheria za Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano(TEHAMA) na Mkuu wa Idara ya Mafunzo Chuo Kikuu Mzumbe, Dk Ubena
John, Mchumi Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jasson Bagonza, Mkurugenzi wa
Utawala na Rasilimali watu wa Benki ya TIB, Stella Nghambi.
Wajumbe wengine ni Mwanzilishi na Mkurugenzi wa
Inonovex, Leonard Kitoka, aliyekuwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Posta
Tanzania, Zanzibar, Fatma Juma Bakari na Mratibu Mkazi wa Misaada ya
No comments:
Post a Comment