Monday, October 10, 2016

Ethiopia yatangaza hali ya tahadhari ya miezi 6

Raia wa Ethiopia wakifanya maandamano.Serikali ya taifa hilo imetangaza hali ya tahadhari ya miezi sita kufuatia maandamano hayo
Serikali ya Ethiopia imetangaza hali ya dharura kwa miezi sita.
Tangazo hilo limetolewa baada ya miezi kadha ya maandamano dhidi ya serikali, yaliyofanywa na makabila mawili makubwa ya Ethiopia ya Oromo na Amhara.
Makabila hayo yanalalamika kuwa yametengwa kiuchumi na kisiasa.
Ghasia baina ya waandamanaji na polisi zilizidi tangu watu 55 walipokufa katika sherehe za kitamaduni za Oromo, Jumapili iliyopita.
Mashirika ya kutetea haki za kibinaadamu yanasema, mamia ya watu wameuawa, na maelfu kukamatwa tangu maandamano yalipoanza

No comments:

Post a Comment