Rais wa colombia Juan Manuel Santos
amesema kuwa atatoa pesa kutoka katika tuzo yake ya amani ya Nobel ili
kuwasaidia waathirika wa mgogoro katika nchi yake. Alipata tuzo hiyo
kutokana na juhudi zake za makubaliano ya amani na kundi la kigaidi la
FARC.
Santos na kiongozi wa kundi hilo Timochenko walisaini
makubaliano ya amani mwezi uliopita ili kumaliza mgogoro wa zaidi ya
miongo miwili. Lakini wananchi wa Colombia walipiga kura ya hapana juu ya makubaliano hayo. Santos anatarajia kupokea zaidi ya dola mia tisa elfu kutoka kamati ya Nobel.
No comments:
Post a Comment