Kijana
Said Mrisho anayedaiwa kujeruhiwa na kutobolewa macho na Salumu
Henjelewe maarufu kama Scorpion (katikati), akisaidiwa na ndugu zake
wakati akiingia ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda
kuzungumza na waandishi wa habari.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia), akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari kabla ya kumpa fursa kijana Said
kuzungumza na wanahabari.
Kijana Said Mrisho (kulia), akizungumza na wanahabari. Kulia kwake ni mke wake Stara Soud.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiwa ameinama kwa uchungu wakati kijana huyo alipokuwa akizungumza na wanahabari.
Kijana
Said Mrisho anayedaiwa kujeruhiwa na kutobolewa macho na Salumu
Henjelewe maarufu kama Scorpion (kulia), akilia kwa uchungu wakati
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mbele ya Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo. Kushoto ni mke wake, Stara Soud
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magembe (kushoto), akimfariji kijana Said Mrisho.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimfariji kijana Said Mrisho.
Mama yake Said Mrisho, Halima Lwiza Abdallah akilia.
Ndugu
zake Said Mrisho wakitoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam baada
ya kuzungumza na wanahabari. Kushoto mbele ni mama yake Said, Halima
Lwiza Abdallah na kulia ni mke wake, Stara Soud.
Said Mrisho akisaidiwa kushuka ngazi wakati akitoka kuzungumza na wanahabari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Na Dotto Mwaibale
MAJONZI
na vilio vilitawala ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda wakati kijna Said Mrisho anayedaiwa kujeruhiwa na kutobolewa
macho na Salumu Henjelewe maarufu kama 'Scorpion' Buguruni Sheli
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mbele ya Mkuu wa Mkoa Dar
es Salaam leo asubuhi kuwa hata ona tena katika maisha yake kufuatia
kujeruhiwa vibaya kwenye mishipa ya macho na mtuhumiwa huyo na kupoteza
uwezekano wa kuona.
"Nilijua
ipo siku moja nitakufa lakini sikutegemea kuwa nitakuja kutolewa macho
yangu kikatili kiasi hiki sijui Mungu anampango gani na mimi wala sijui
nini ya hatima ya maisha yangu" alisema Mrisho ambapo ukumbi mzima
uligubikwa na ukimya sanjari na simanzi, huku mke wake Stara Soud
akishindwa kujizuia kulia.
Mrisho
alisema anamshukuru sana Rais John Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda kwa jitihada walizofanya za kumsaidia kupata
matibabu lakini imeshindika kwa kuwa mishipa yote yenye uwezo wa
kumfanya aweze kuona imeharibiwa vibaya na mtuhumiwa huyo hivyo hataweza
kuona tena katika maisha yake.
"Iwapo
kama mishipa isingeharibiwa kwa visu mama yangu kipenzi Halima Lwiza
Abdallah alikuwa yupo tayari kutoa jicho lake moja kwa ajili ya
kunisaidia niweze kuona lakini kwa bahati mbaya hilo halitawezekana
baada ya madaktari kunieleza kuwa mishipa ya macho yangu imeharibiwa"
alisema Mrisho kwa huzuni na kuanza kulia.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wamepokea kwa huzuni
taarifa hiyo ya madaktari na kumuomba Mrisho asikate tamaa kwani
serikali itaangalia jinsi ya kumsaidia.
Makonda
alisema serikali itatoa sh.milioni 10 kama mtaji ili ziweze kumsaidia
wakati wakiangalia namna ya kuwashirikisha watu wengine kwa ajili ya
kumsaidia.
Makonda
alisema Serikali itamsaidia kufanyiwa upasuaji wa kuwekewa macho ya
bandia ili awe katika mwonekano wa kawaida ingawa atakuwa haoni.
"Pamoja
na kumpatia kiasi hicho cha fedha katika kipindi hiki cha mpito ambacho
atakuwa akihitaji kwenda katika matibabu na sehemu zingine tutakuwa
tukimsaidia usafari wa kwenda maeneo hayo" alisema Makonda.(Imeandaliwa na Dotto Mwaibale)
No comments:
Post a Comment