Mwakilishi
wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi na Mbunge wa Jimbo hilo Mh.
Bahati Ali Abeid Nyuma ya Balozi wakimkabidhi Madeski 50, Mashine ya
Fotokopi na Printer Kaimu Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Msingi ya Mangapwani
Mwalimu Said Abass Othman. Wa kwanza kutoka Kushoto ni Mke wa
Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Mama Asha Suleiman Iddi na Mkuu wa Wilaya
ya Kaskazini “B” Nd. Issa Juma. (Picha zote na Hassan Issa – OMPR – ZNZ)
Mbunge
wa Jimbo la Mahonda Mh. Bahati Ali Abeid akitoa ahadi kwa walimu na
wanafunzi wa Skuli ya Msingi Mangapwani ya kusaidia ujenzi wa mnara wa
Tangfi la Maji kwenye Kisima cha Skuli hiyo ili kuwaondoshea usum,bufu
wanafunzi wake. Mkurugenzi wa Idara ya Elimu, Maandalizi na Msingi, Bibi Safia Ali Rijali akiushukuru Uongozi wa Jimbo la Mahonda kwa hatua unaochukuwa wa kusaidia sekta ya elimu.
Baadhi ya Wanafunzi wa Skuli ya Msingi ya Mangapwani wakishuhudia hafla ya skuli yao kukabidhiwa madeski 50 kutoka kwa Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif hayupo pichani yaliyotolewa msaada ya Kampuni ya Simu ya Tigo.
Baadhi ya Madeski 50 yaliyokabidhiwa skuli ya msingi Mangapwani kutoka kwa Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif kwa msaada wa Kampuni ya Tigo.
Mwakilishi
wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi akikabidhi Shilingi Milioni
1,000,000/- kwa Mshika Fedha wa Kikundi cha Ushirika cha Msitupumbaze
cha Mtaa wa Kiduka Njaa Mangapwani Bibi Asha Muhsin Hassan kukamilisha
ahadi aliyotoa wiki iliyopita ya kusaidia kukamilisha jengo la ufugaji
wa mbuzi wa maziwa la wanaushirika hao.
Na Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
07/10/2016.
MAKAMU
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amemuonya Mtu
aliyeamua kuvamia Eneo la Skuli ya Msingi ya Mangapwani kwa ajili ya
Ujenzi wa Nyumba kuacha mara moja mpango huo ili kuepuka hasara
inayoweza kumtokea hapo baadaye.
Alisema
Serikali kupitia Taasisi zake zinazosimamia ujenzi na masuala ya
Ardhi hazitasita kumvunjia mtu huyo endapo ataamua kukaidi onyo hilo
kutokana na kuonyesha dalili za mapema za kuweka mawe kwenye eneo hilo
kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi huo.
Balozi
Seif Ali Iddi alitoa onyo hilo wakati akikabidhi Madeski 50 yenye
Thamani ya Shilingi Milioni 9,000,000/- aliyopewa Msaada na Uongozi wa
Kampuni ya Mtandao wa Simu za Mkononi wa Tigo kwa ajili ya Skuli ya
Msingi Mangapwani ndani ya Jimbo la Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Balozi
Seif katika hafla hiyo pia akakabidhi msaada wa Mashine Moja ya
Fotokopi na Mbunge wa Jimbo hilo la Mahonda Mh. Bahati Ali Abeid
akakabidhi msaada wa Kompyuta Moja na Printa yake kwa Skuli hiyo vyote
vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 4,540,000/.
Alisema
tabia ya baadhi ya Watu kuamua kuvamia maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya
shughuli za Kijamii kama Vituo vya Afya na Skuli inayoonekana
kuongezeka kila siku katika maeneo mbali mbali hapa nchini inaondosha
utulivu wa walimu na wanafunzi kiasi kwamba kwa sasa inastahiki
kudhibitiwa.
Balozi
Seif alisema Ardhi ni mali ya Serikali, hivyo Taasisi zinazosimamia
ardhi na Mipango Miji ndizo zenye jukumu na wajibu wa kupima maeneo yote
na baadaye kuyagawa kwa Wananchi na Miradi ya Jamii kwa mujibu wa
mahitaji halisi ya matumizi ya ardhi husika.
Katika
kuunga mkono jitihada za Walimu, Wanafunzi na Kamati ya Skuli ya Msingi
Mangapwani Mwakilishi huyo wa Jimbo la Mahonda ameahidi kutoa mchango
wa Kompyuta Mbili zitakazowasaidia walimu na wanafunzi hao katika masomo
yao ili kwenda sambamba na mabadiliko ya sasa ya sayansi na Teknolojia.
Naye
Mbunge wa Jimbo la Mahonda Mh. Bahati Ali Abeid aliuagiza Uongozi wa
Kamati ya Skuli ya Msingi Mangapwani kushirikiana na Sheha wa Shehia
hiyo kuanza hatua za awali za kutafuta Hati Miliki ya Eneo la Skuli hiyo
na uongozi wa Jimbo hilo utakuwa tayari kusaidia nguvu za uwezeshaji
katika upatikanaji wa Hati Miliki hiyo.
Mh.
Bahati alisema udhaifu mwingi unaoendelea kufanywa na baadhi ya Kamati
za Skuli mbali mbali Nchini ndio unaotoa mwanya kwa wajanja kuzaa mbinu
za kushirikiana na matapeli mitaani kuuza au kukata viwanja ndani ya
Maeneo yaliyotengwa na Serikali kwa shughuli maalum za Kijamii.
Mbunge
huyo wa Jimbo la Mahonda katika kuchangia nguvu za kupunguza changamoto
zinazoikabili skuli hiyo ya msingi Mangapwani likiwemo tatizo la
huduma za maji safi na salama aliahidi kusaidia fedha kwa ajili ya
ujenzi wa Mnara wa Tangi kwenye Kisima kilichopo ndani ya Skuli hiyo.
Akitoa
shukrani kwa niaba ya Wizara ya Elimu pamoja na Skuli ya Msingi
Mangapwani, Mkurugenzi wa Idara ya Elimu, Maandalizi na Msingi Bibi
Safia Ali Rijali alisema jamii imekuwa ikishuhudia na kufarajika
kutokana na kasi kubwa inayofanywa na Balozi Seif Ali Iddi katika
kusaidia sekta ya Elimu.
Mkurugenzi
Safia alisema jitihada zinazochukuliwa na Viongozi, wahisani pamoja na
wananchi katika kuunga mkono mapambano dhidi ya kuzitafutia ufumbuzi
changamoto za Sekta ya Elimu zinatoa mwanga wa kusaidia Watoto katika
kujitafutia Taalum inayokubalika.
Alisema
nguvu za utengenezwaji wa madeski katika maeneo tofauti nchini
zinazofanywa na Viongozi hao pamoja na washirika wa maendeleo zinawapa
fursa nzuri walimu kuwasomesha wanafunzi wao katika utulivu mkubwa.
Skuli
ya Msingi Mangapwani yenye Madarasa kuanzia la kwanza hadi la saba
iliyofungulia rasmi Tarehe 3 Septemba mwaka 2007 na wanafunzi wake
kuanza kufanya Mitihani ya Taifa ya Darasa la Saba kuanzia mwaka 2011
hivi sasa ni miongoni mwa skuli ya Msingi Wilaya ya Kaskazini “B”
inayofanya vizuri katika kutoa wanafunzi wa mchepuo wa darasa la Tisa.
No comments:
Post a Comment