Saturday, October 8, 2016

MAJERUHI WA KUTOBOLEWA MACHO KIKATILI NA SCORPION ASEMA HATAWEZA KUONA TENA


Kijana Said Mrisho anayedaiwa kujeruhiwa na kutobolewa macho na Salumu Henjelewe maarufu kama Scorpion (katikati), akisaidiwa na ndugu zake wakati akiingia ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda kuzungumza na waandishi wa habari.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kabla ya kumpa fursa kijana Said kuzungumza na wanahabari.
Kijana Said Mrisho (kulia), akizungumza na wanahabari. Kulia kwake ni mke wake Stara Soud.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiwa ameinama kwa uchungu wakati kijana huyo alipokuwa akizungumza na wanahabari.
Kijana Said Mrisho anayedaiwa kujeruhiwa na kutobolewa macho na Salumu Henjelewe maarufu kama Scorpion (kulia), akilia kwa uchungu wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo. Kushoto ni mke wake, Stara Soud
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magembe (kushoto), akimfariji kijana Said Mrisho.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimfariji kijana Said Mrisho.
Mama yake Said Mrisho, Halima Lwiza Abdallah  akilia.
Ndugu zake Said Mrisho wakitoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kuzungumza na wanahabari. Kushoto mbele ni mama yake Said, Halima Lwiza Abdallah  na kulia ni mke wake, Stara Soud.
Said Mrisho akisaidiwa kushuka ngazi wakati akitoka kuzungumza na wanahabari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Na Dotto Mwaibale
MAJONZI na vilio vilitawala ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati kijna Said Mrisho anayedaiwa kujeruhiwa na kutobolewa macho na Salumu Henjelewe maarufu kama 'Scorpion' Buguruni Sheli alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mbele ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam leo asubuhi kuwa hata ona tena katika maisha yake kufuatia kujeruhiwa vibaya kwenye mishipa ya macho na mtuhumiwa huyo na kupoteza uwezekano wa kuona.

"Nilijua ipo siku moja nitakufa lakini sikutegemea kuwa nitakuja kutolewa macho yangu kikatili kiasi hiki sijui Mungu anampango gani na mimi wala sijui nini ya hatima ya maisha yangu" alisema Mrisho ambapo ukumbi mzima uligubikwa na ukimya sanjari na simanzi, huku mke wake Stara Soud akishindwa kujizuia kulia.

Mrisho alisema anamshukuru sana Rais John Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa jitihada walizofanya za kumsaidia kupata matibabu lakini imeshindika kwa kuwa mishipa yote yenye uwezo wa kumfanya aweze kuona imeharibiwa vibaya na mtuhumiwa huyo hivyo hataweza kuona tena katika maisha yake.

"Iwapo kama mishipa isingeharibiwa kwa visu mama yangu kipenzi Halima Lwiza Abdallah alikuwa yupo tayari kutoa jicho lake moja kwa ajili ya kunisaidia niweze kuona lakini kwa bahati mbaya hilo halitawezekana baada ya madaktari kunieleza kuwa mishipa ya macho yangu imeharibiwa" alisema Mrisho kwa huzuni na kuanza kulia.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wamepokea kwa huzuni taarifa hiyo ya madaktari na kumuomba Mrisho asikate tamaa kwani serikali itaangalia jinsi ya kumsaidia.

Makonda alisema serikali itatoa sh.milioni 10 kama mtaji ili ziweze kumsaidia wakati wakiangalia namna ya kuwashirikisha watu wengine kwa ajili ya kumsaidia.

Makonda alisema Serikali itamsaidia kufanyiwa upasuaji wa kuwekewa macho ya bandia ili awe katika mwonekano wa kawaida ingawa atakuwa haoni.

"Pamoja na kumpatia kiasi hicho cha fedha katika kipindi hiki cha mpito ambacho atakuwa akihitaji kwenda katika matibabu na sehemu zingine tutakuwa tukimsaidia usafari wa kwenda maeneo hayo" alisema Makonda.(Imeandaliwa na Dotto Mwaibale)

No comments:

Post a Comment