Mbunge
wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akimkabidhi mganga mkuu wa
zahanati ya Mtamaa Bw Godson Charles Swai kifaa maalumu kwa ajili ya
kipimo cha ugonjwa wa Malaria
Mashine ya Kupima Maralia (Binocular Microscope) Mega 7 ikiwa imefunguliwa kwenye Boksi maalumu ili wananchi waione kwa karibu
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mtamaa kupitia mkutano wa hadhara
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wake
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima
Shukrani na Pongezi
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akishiriki kucheza ngoma ya Kinyaturu
Mbunge
wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akisaini kitabu cha wageni mara
baada ya kuwasili Kijijini Mtamaa kwa ajili ya mkutano na kukabidhi
kifaa maalumu kwa ajili ya kupimia Malaria
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Mtamaa
Baadhi ya wananchi wakifurahia kifaa cha kupimia Malaria
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Mbua Gwae Chima akisisitiza jambo wakati wa Mkutano
Mbunge wa Jimbo la
Singida Mjini Mussa Sima ameadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere kwa kuwarahisishia huduma za upimaji wa Maralia wananchi wa
Kijiji cha Mtamaa.
Tatizo hilo sugu
limepatiwa ufumbuzi mara baada ya Mbunge huyo kuwapatia Mashine ya Kupima
Maralia (Binocular Microscope) Mega 7 iliyonunuliwa kwa gharama ya zaidi ya
shilingi milioni mbili nchini Kenya.
Mhe Sima amemkabidhi
mashine hiyo Mganga Mkuu wa Zahanati ya Mtamaa Godson Charles Swai mara baada
ya mkutano wake na wananchi wa kijiji hicho ambapo pia ametumia mkutano huo
kuwashukuru wananchi hao kwa kumchagua kuwa Mbunge wa Jimbo hilo kwenye
uchaguzi mkuu uliofanyika Octoba Mwaka jana.
Sima alisema kuwa ameamua
kuitumia siku hii ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere kwani wakati wa utawala wake
alisisitiza uwajibikaji kwa viongozi kwa kuwatumikia zaidi wananchi kuliko
kujilimbikizia mali.
Sima Alisema kuwa Mwalimu
Nyerere atakumbukwa zaidi kwa kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kuwaunganisha
watanzania, kutetea usalama wa taifa katika vita vya Kagera dhidi ya Nduli idd
Amin, na kufanya uhuru wa kazi na uhuru wa maendeleo.
Alisema kuwa Mwalimu
Nyerere katika mambo aliyoyaamini sana na kuyapa mkazo ni pamoja na kupamabana
na masuala ya haki usawa kwani alijenga imani katika misingi ya utu,haki na
usawa kwa kila Raia wa Tanzania.
Sima ameahidi kuendelea
kufanya mikutano mingi katika maeneo mbalimbali ya Jimbo lake ili kuelezea
namna ilani ya uchaguzi inavyotekelezwa kwa vitendo sambamba na kushiriki
shughuli za maendendeleo ya wananchi.
Kuhusu kadhia ya uduni wa
upatikanaji wa Maji katika Kijiji cha Mtamaa A Mbunge huyo amesema kuwa hadi
kufikia mwezi aprili mwakani maji yatakuwa yameanza kutoka ili kumaliza kadhia
hiyo kwani mradi mkubwa wa maji utakuwa umemalizika.
Kwa upande wake Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Singida Mbua Gwae Chima ambaye pia ni Diwani wa Kata ya
Mtamaa ametoa shukrani zake kwa mbunge huyo kwa kufanya mkutano wa tatu katika
eneo hilo tangu aingie madarakani huku akiwasaidia wananchi katika kuboresha
shughuli za maendeleo.
Chima amesema kuwa Mbunge
huyo ni muwakilishi mzuri wa shughuli za wananchi wake na ameonyesha uwezo
mkubwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutetea hoja na
kusimamia misingi ya uwajibikaji.
Naye mganga mkuu wa
zahanati ya Mtamaa Bw Godson Charles Swai amesema kuwa kifaa hicho maalumu
kilichotolewa kwa ajili ya upimaji wa Malaria ni madhubuti na imara hivyo
kinatarajia kuwasaidia wananchi wengi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakisafiri
umbali wa karibu kilomita 20 kwenda kupima ugonjwa huo.
Hayati Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere alizaliwa tarehe 13, April 1922 katika Kijiji cha Butiama
Wilaya ya Musoma Mkoani Mara.
Maadhimisho ya Mwalimu
Nyerere hufanyika kila mwaka ambapo watanzania popote ulimwenguni huadhimisha
kwa sala na matembezi mbalimbali kama ishara ya heshima kwa muasisi wa Taifa
lao.
No comments:
Post a Comment