Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Naibu Waziri wa Biashara kutoka Jamhuri ya Watu wa China
Qian Keming aliyefika Ikulu pamoja na ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.
. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu youqing Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Waziri wa Biashara kutoka Jamhuri ya Watu wa China Qian Keming .
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Makamu wa Rais wa Benki ya EXIM ya China Sun Ping ambaye
aliambatana na Naibu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China
Qian Keming, pamoja na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu youqing.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Biashara kutoka Jamhuri ya
Watu wa China Qian Keming watatu kutoka kulia aliyefika
Ikulu pamoja na ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo. Wengine katika
picha ni Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango wakwanza
(kushoto) Makamu wa Rais wa Benki ya EXIM ya China Sun Ping wapili
kutoka (kushoto) Balozi wa China hapa nchini Dkt. Dkt. Lu youqing watatu
kutoka (kushoto),Pamoja na Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage wapili kutoka kulia.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
Naibu Waziri wa Biashara kutoka Jamhuri ya Watu wa China Qian Keming
mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Balozi wa China hapa nchini Dkt.
Lu youqing mara baada ya kumaliza mazungumzo ya pamoja na ujumbe wa
Naibu Waziri wa Biashara kutoka Jamhuri ya Watu wa Jamhuri ya China
uliofika Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akijadiliana jambo na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu youqing mara
baada ya kumaliza mazungumzo ya pamoja na ujumbe wa Naibu Waziri wa
Biashara kutoka Jamhuri ya Watu wa Jamhuri ya China uliofika Ikulu
jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU,
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 14 Oktoba,
2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya
Watu wa China Mhe.Qian Keming ambapo viongozi hao wamekubaliana kuharakisha
miradi inayotekelezwa kwa ushirikiano wa nchi hizo mbili ukiwemo mradi wa
ujenzi wa reli ya kati.
Katika
mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam Rais Magufuli
amemueleza Mhe. Qian Keming kuwa Serikali yake ya awamu ya tano inataka kuona
mambo yakifanyika na kutoa matokeo bila kupoteza muda na kwamba angependa wadau
wa maendeleo hasa nchi ya China ambayo ni ndugu na rafiki mkubwa wa Tanzania iende
katika kasi hiyo hiyo.
Rais Magufuli
ameuzungumzia mradi wa ujenzi wa reli ya kati ya kutoka Dar es Salaam, Mwanza,
Kigoma na kuunganisha nchi za Rwanda na Burundi ambao Tanzania imetenga
Shilingi Trilioni moja kwa ajili ya kuanza ujenzi katika bajeti hii, kwa kutaka
China ambayo imekubali kushiriki katika ujenzi iendane na kasi ya Serikali
yake.
“Mhe. Qian
Keming sisi tumeamua kuanza ujenzi na tayari Wakandarasi 32 wamejitokeza kuomba
kujenga reli ya kati kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro umbali wa kilometa 200
za mwanzo na tutatumia fedha zetu wenyewe.
“Kazi hii
tunataka ianze mwaka huu wa fedha, kwa sababu upembuzi yakinifu na usanifu
umeshafanyika, kwa hiyo na nyie ongezeni kasi ili mradi huu wote ukamilike,
nataka uwe umekamilika kabla sijaondoka madarakani” amesema Rais
Magufuli.
Dkt. Magufuli
ameongeza kuwa mradi huo una manufaa makubwa kwa Tanzania na nchi nyingine nane
zinazotegemea bandari ya Dar es Salaam na kwamba kukamilika kwake kutatoa
mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania ambayo imedharia kuwa nchi
ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
Kwa upande
wake Naibu Waziri wa Biashara wa China Mheshimiwa Qian Keming amempongeza Rais
Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kukuza uchumi wa Tanzania, kupiga vita
rushwa na kwa namna ya kipekee kwa dhamira yake ya kuimarisha zaidi uhusiano na
ushirikiano na China na ameahidi kuwa Serikali ya China itaongeza msukumo
katika uharakishaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa
reli ya kati.
“Mheshimiwa
Rais Magufuli nimeielewa dhamira yako na kiu uliyonayo, naona kabisa kwamba dhamira
ya kisiasa ipo ya kutosha, tunachotakiwa kukifanya ni kuwasukuma wataalamu wetu
waongeze kasi, na mimi nakuahidi kuwa tulikuwa tunakwenda kwa kasi ya kilometa
100 kwa saa, sasa tutaongeza na kwenda kilometa 200 kwa saa” amesema Mhe.
Qian Keming.
Mazungumzo
hayo yamehudhuriwa na Balozi wa China hapa nchini Mhe. Dkt. Lu Youqing, Makamu
wa Rais wa Benki ya Exim ya China Bw. Sun Ping, Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji Mhe. Charles John Mwijage na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip
Mpango.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa
Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
14 Oktoba,
2016
No comments:
Post a Comment