Mtendaji Mkuu TEMESA Dr. Mussa Mgwatu (katikati) akikagua chumba maalumu kwa ajili ya injini (Engine Room) kulia ni msaidizi wa Meneja Bw. Charles Mbegete na kushoto ni Kaimu Meneja TEMESA Kagera Bw. Wilson Nyitwa.
Mtendaji Mkuu TEMESA Dr. Mussa Mgwatu (wa tatu kushoto) akiongea na baadhi ya watumishi wa TEMESA Kagera alipotembelea kituoni hapo kukagua jinsi Ofisi inavyofanya kazi na kuzungumza na wafanyakazi.
Na Theresia Mwami TEMESA Kagera
MTENDAJI
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu amewataka
watumishi wake kuacha kufanya kazi kwa uzembe na mazoea badala yake
waongeze ubunifu katika miundombinu iliyopo ili kuweza kuzalisha zaidi
ikiwa ni sanjali na kuweka mikakati madhubuti ya kukusanya madeni siku
hadi siku.
Ameota
agizo hilo alipotembelea na kujionea hali ya karakana ya TEMESA mkoani
Kagera na kumuagiza Kaimu Meneja wa TEMESA Kagera Bw.Wilson Nyitwa
kusimamia kwa makini utekelezaji wa majukumu ya Wakala huo mkoani hapo.
“Inatupasa
kuanza na hiki kidogo tulicho nacho kwa kuziba mianya ya uzembe na
muongeze uadilifu na ufuatiliaji katika kazi tulizo nazo tufanikishe
utendaji wa kazi zetu” alisema Dkt. Mgwatu.
Dkt
Mussa Mgwatu ameongeza kuwa watendaji wanapaswa kupambana ili kulinda
soko lililopo kwa sasa na hata kuongeza wateja zaidi. Kwa sasa wateja wa
TEMESA ni taasisi za serikali ambazo zinapeleka magari na mitambo
kutengenezwa katika karakana zao.
Aidha kwa upande wake Kaimu Meneja wa TEMESA Kagera Bw.Wilson Nyitwa alieleza kuwa Kituo chake mbali
na kuwa na karakana na kutengeneza magari na vifaa vya
umeme,kukodishaji mitambo na usimikaji umeme katika majengo mbali mbali
ya serikali pia kinasimamia uendeshaji wa vivuko viwili vilivyopo
Kyanyabasa na Ruvuvu.
Alieleza
kuwa TEMESA Kagera ina changamoto nyingi zikiwemo uchakavu wa Karakana
yake iliyojengwa tangu mwaka 1958 pamoja na kukosa vitendea kazi muhimu
pamoja na magari kwa ajili ya matumizi ya ofisi lakini bado wanafanya
kazi kwa kujituma na kuzalisha zaidi ya Shillingi Million 50 kwa mwezi.
“Nakuomba
Mtendaji Mkuu utusaidie gari moja kwa ajili ya matumizi ya kituo
nyongeza ya mafundi, vitendea kazi vya kisasa vya karakana ,ukarabati wa
karakana ya mkoa ili kutuwezesha kutekeleza majukumu yetu na kuzalisha
zaidi.
Mtendaji
Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu yupo katika ziara ya kikazi Kanda ya
Ziwa na atatembelea vituo vya TEMESA vilivyopo ili kubaini changamoto na
kujionea utendaji kazi wa vituo hivyo na kwa kuanzia yupo Mkoani
Kagera.
No comments:
Post a Comment