WAZEE WASTAAFU WANAWEZA KUWA MABILIONEA NA KUIBADILISHA NCHI
Kaimu Mkuu wa wilaya ya Lushoto
ambaye ni Afisa Tarafa ya Lushoto, Asha Kikoti akifungua mkutano wa
uzinduzi wa chama cha wazee wastaafu wilayani Lushoto kushoto ni
MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF
hapa nchini, Adam Mayingu kulia kwake ni Mwenyekiti wa Chama cha Wazee
wilayani humo Paul Kirua.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF
hapa nchini, Adam Mayingu akizungumza na wazee wastaafu wilayani
Lushoto.
|
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF
hapa nchini, Adam Mayingu akizungumza na wazee wastaafu wilayani
Lushoto.
Meneja Matekelezo wa PSPF Franscis Mselemu akizungumza jambo
wakati wa uzinduzi wa chama hicho kulia kwake ni MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF
hapa nchini, Adam Mayingu.
|
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF
hapa nchini, Adam Mayingu akimkabidhi Katibu Mkuu wa Chama cha wazee
Wastaafu wilayani Lushoto (Chawasewili) Paul Kirua katiba ya Chama hicho
mara baada ya kukizundua kushoto ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya
Lushoto, Asha Kikoti.
Katibu Mkuu wa Chama cha wazee Wastaafu wilayani Lushoto (Chawasewili)
Paul Kirua akionyesha juu katiba ya Chama hicho mara baada ya
kukizunduawilayani humo kushoto ni MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa
Pensheni wa PSPF
hapa nchini, Adam Mayingu.
Wazee Wastaafu wilayani Lushoto wakimsikiliza kwa umakini
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF
hapa nchini, Adam Mayingu.
|
Mmoja kati ya Wazee Wastaafu wilayani Lushoto, Yohana Wiliamu
akiuliza swali katika mkutano huo wa uzinduzi wa chama hicho.
|
Mzee Mstaafu wilayani Lushoto, Judica Mandia akiuliza
swali kwenye mkutano huo.
|
Juma
Rashidi ambaye ni miuongoni mwa wazee wastaafu wilayani Lushoto
akiuliza swali kwa mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa
PSPF, Adam Mayingu.
|
MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF
hapa nchini, Adam Mayingu amesema kuwa wazee wastaafu wanauwezo wa kuwa
mabilionea na kuibadilisha nchi kwa kutengeneza ajira ,kubuni miradi inayoweza
kuwaingizia kipato baada ya kulitumikia taifa katika nafasi mbalimbali
walizokuwa nazo.
Alisema kwani asilimia kubwa wanaweza
kuanzisha miradi mbalimbali ambayo inaweza kuwasaidia kujiongezea kipato hali
itakayopelekea vijana kuweza kuinua maisha yao kitendo ambacho pia kitasaidia
kuongeza pato la serikali.
Mayingu aliyasema hayo wakati wa wiki
ya huduma kwa wateja Duniani ambapo mfuko huo unakutana na wadau wake ili
kuweza kubaini changamoto ambazo ikiwemo kuangalia namna ya
kukabiliana nazo.
Wiki hiyo ilikwenda sambamba na
uzinduzi wa chama cha wazee wastaafu wilayani Lushoto (Chawisewilu) chenye
makazi yake mjini hapa waliokuwa wakifanya kazi na baadae kustaafu waliweza
kuhudhuriwa kwa wingi na kutoa mapendekezo yao.
“Ukiangalia wazee wastaafu wanapokuwa wamepata fedha zao za kiunua
mgongo badala ya kwenda kuzitumia katika matumizi yasiyokuwa ya lazima badala
yake waone namna ya kuzitumia kubuni miradi itakayokuwa chachu kwao kupitia
hatua kubwa za kimaendeleo “Alisema.
“Sisi kama Mfuko wa Pensheni wa PSPF
tunaunga mkono chama chenu lakini pia niwaambie Sido wapo tuzungumze nao
ikiwemo kuweka utaratibu mzuri ili muweza kuona namna ya kuweza kunufaika na
uwepo wao “Alisema.
“Lakini pia msisite kuwatumia wataalamu
kwenye masuala mbalimbali ya ujasiriamali kwani hiyo ndio njia ambayo inaweza
kuwa chachu ya kuweza kufikia malengo yenu hasa katika kipindi hiki kwa
kushirikiana “Alisema.
Aidha pia aliwataka kupitia umoja wao
kutumia fursa nyingi zilizopo kwenye maeneo yao kwani wanao umri wa kuishi
mkubwa badala yake yaondokana na dhani ya kuwa watu wanapokuwa wakistaafu
wanafariki kitendo ambacho sio hakina ukweli wowote.
Lakini pia aliwataka kutumia fursa hiyo
waliyoipata kuieli misha jamii huku akiwaomba kupitia chama chao kuwahimiza
vijana wao kujiunga ma mfuko wa Pensheni wa PSPF ili waweze kunufaika na mafao
yanayotolewa.
Awali akizungumza wakati akifungua
kikao hicho,Kaimu Mkuu wa wilaya ya Lushoto, Asha Kikoti aliwataka wazee wastafu
kuhakikisha fedha wanazozipata za kiunua mgongo kuweka mpango mzuri wa kuzitumia
kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo ili waweze kujiingizia
kipato.
“Kiuhalisia wazee wastaafu wanapopata fedha zao wanaona kama vile ni
nyingi na kuzitumia bila kwa haraka bila kufikiria hata kuzianzishia miradi
ambayo inaweza kuwasaidia kupambana na ukali wa maisha “Alisema huku
akiwasisitizia wabadilike.
Sambamba na hayo aliwataka pia kuwa na
mpango mzuri wa matumizi ya fedha zao za kiinua mgongo ili ziweze kuwasaidia
kutumiza ndoto zao katika maisha ikiwemo kuwa na maisha
mazuri.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
No comments:
Post a Comment