Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ( katikati) akicheza moja ya ngoma za kiutamaduni wakati wa kufunga Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016 liliofanyika wilayani Rungwe mkoani Mbeya leo Oktoba 08,2016 kulia ni Naibu Spika Mhe. Tulia Ackson na kushoto ni Katibu Mtendaji BASATA Geodfrey Mngereza.
Kikundi cha Utamaduni cha Ikama kikitoa burudani wakati wa kufunga Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016 liliofanyika wilayani Rungwe mkoani Mbeya leo Oktoba 08,2016.
Kikundi
cha Utamaduni cha Ikama kikitoa burudani wakati wa kufunga Tamasha la
Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016 liliofanyika wilayani Rungwe
mkoani Mbeya leo Oktoba 08,2016. (Picha zote/Habari na Kitengo cha Mawasiliano WHUSM)
WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amewashauri vijana kutumia ngoma za asili kujiajiri kwani ni fursa mojawapo ya ajira kwa sasa.
Ametoa
ushauri huo leo Mjini Mbeya alipokuwa akifunga Tamasha la Utamaduni la
Tulia Tradition Festival 2016 na kuwahimiza vijana kutosubiri kuajiriwa
ikiwa wanaona wana uwezo wa kufanya kitu ambacho kitawasaidia kupata
kipato na kuendesha maisha yao.
“Ngoma
za asili ni chanzo cha ajira kwa vijana na sisi kama Serikali
tutashirikiana na wadau wa Sanaa na Utamaduni ili kutengeneza ajira na
kudumisha mila na desturi za nchi yetu” alisistiza Mhe. Nnauye.
Aidha
kwa upande wake Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Tulia Ackson amesema kuwa fursa pekee kwa vijana kujiajiri kupitia
shughuli za Sanaa na Utamaduni kwani ndio sekta ambazo zimetoa ajira
kwa vijana wengi duniani kwa sasa.
“Nawashauri
vijana wa kitanzania kuangalia na upande huu wa Sanaa na Utamaduni kuna
ajira pia na sisi tupo pamoja nao na tutawapa ushirikiano ili wafikie malengo” alisema Mhe. Tulia.
Tamasha
hili liliondaliwa na Naibu Spika Mhe.Tulia Ackson linafanyika kwa siku
mbili na limeshirikisha vikundi vya ngoma za asili vipatavyo 62 kutoka
mkoani Mbeya.
No comments:
Post a Comment