Kampeni ya 'DEBE NA JEMBE' kikazi zaidi...kule Joha Ngasa huku Mansour Jumanne. |
NA ALBERT G. SENGO: MWANZA
Watangazaji
na Ma-Dj wa kituo cha redio Jembe Fm 93.7 cha jijini Mwanza, tangu siku
ya Jumatatu ya tarehe 2 mwezi October mwaka huu 2016 wako katika
ushindani mkali katika kupiga debe kwenye daladala za ndani na nje ya
jiji la Mwanza ambapo wamegeuka kuwa kivutio cha kutosha kwa abiria
wanaotumia usafiri huo pamoja na watembea kwa miguu kwenye vituo
mbalimbali vya daladala na waskilizaji, kwani ubunifu wao umegeuka kuwa
burudani na siyo kazi ya kuchosha kama wengi wanavyoichulia.
"Ni
kama vile waliingia darasani kujifunza mbinu za kuita wateja na jinsi ya
kuvitaja vituo mbalimbali vya Mwanza, mimi nimewapenda na huwezi
kuamini kama ni wao tunaowasikiliza kupitia vipindi vyao vye wingi
ubunifu, sikudhani kama nitawaona vijana kama wao walio nadhifu
wakifanya kazi hii ambayo wengi tunaidharau, kwa kweli wamenifurahisha"
Alisema Mama Linda Leonard mkazi wa Mabatini jijini Mwanza ambaye
alitumia moja ya daladala ambazo wapiga debe walikuwa watangazaji wa
Jembe Fm.
Abiria
wamesafiri na wanaendelea kusafiri bure huku wakijishindia zawadi,
kupitia daladala tofauti tofauti jijini Mwanza baada ya kulipiwa nauli
na redio Jembe Fm, ambapo wadau mbalimbali na makapuni nao wamehamasika
katika utoaji zawadi na kuisapoti kampeni ya DEBE NA JEMBE baada ya
kuelewa manufaa yake kwa jamii.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza John Mongela naye Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa
Mwanza Ahmed Msangi pamoja na Kitengo cha Polisi Kikosi cha Usalama
barabarani wamesikika mara kadhaa wakihamasisha wananchi ndani ya
kampeni hiyo hasa eneo la Utoaji elimu kwa vijana juu ya kujituma katika
shughuli mbalimbali za kiuchumi, biashara, kujiajiri na ujasiliamali.
Naye
Mkurugenzi wa Jembe Media Group, Kampuni ambayo ndiyo wamiliki wa kituo
hicho cha redio, Dr. Sebastian Ndege almaarufu Dr. Jembe amesema kuwa
kampeni hiyo imeletwa maalum kwa wananchi, wasikilizaji wa Jembe Fm
mkoani Mwanza kama sehemu ya utoaji elimu kwao hasa vijana kuwaimarisha
na kuwafungua kifikra ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha katika suala zima
la kuchapa kazi bila kubagua aina ya kazi au kuchukulia poa shughuli
ndogondogo za kijasiliamali.
"DEBE
NA JEMBE ni Kampeni ya kipekee ambayo imelenga katika kukumbusha na
kuhamasisha uchapakazi au kusema kusema tunataka mtu awe Jembe maana
yake ni kwamba lazima achape kazi" Alisema Dr. Jembe.
Alipoulizwa
kwanini kampeni hiyo imewatumia vijana wake kwenye ushiriki wa nafasi
ya kupiga debe na si nyingine zaidi akasema "Tumechagua nafasi ya kond
(mpiga debe) ikiwa kama sehemu ya kuikumbuka nafasi ya MPIGA DEBE kwenye
daladala kwa sababu ni moja ya kati ya kazi ambazo zimesahaulika au
hazitambuliki kwasababu hazijarasimishwa lakini tukumbuke kwamba MPIGA
DEBE awe kwenye daladala au basi, huyu naye anapata riziki kupitia kazi
halali ambayo kuna wengine wanalisha na kuzisomesha familia zao"
Kisha
akaongeza "Huyu ni bora sana, sana sana...... kuliko mzururaji au yule
kibaka au kijana yeyote anaye bagua kazi ile hali hana chochote mfukoni"
No comments:
Post a Comment