Waziri
wa Mambo ya ndani ya nchi Mh:Mwigulu Nchemba akikagua gwaride la askari
mara baada ya kuwasili makao makuu ya jeshi la polisi zanzibar.
Mapokezi yakiendelea kwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi mara baada ya kuwasili kisiwani Unguja hii leo.
Mwigulu Nchemba akipokea salamu ya utii kutoka kwa askari wa jeshi la polisi hii leo zanzibar.
Mwigulu akisalimiana na baadhi ya viongozi wa jeshi la polisi waliopo visiwani Zanzibar.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi akiongoza kikao cha ndani kilichohusisha viongozi wa juu wa jeshi la polisi Zanzibar.
Mh:Mwigulu
Nchemba akikagua moja ya majengo chakavu yanayohitaji ukarabati ndani
ya eneo la Makao makuu ya jeshi la polisi Unguja.
Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi akiwasili ofisi za Uhamiaji-Zanzibar hii leo.
Mmoja
wa maofisa wa idara ya Uhamiaji akitoa maelezo kwa Waziri Mwigulu
Nchemba namna mchakato wa utoaji wa Vitabu vya kusafiria "Passport"
vinavyotelewa katika ofisi hiyo.
Waziri wa mambo ya ndani akiongoza kikao cha watendaji wa idara ya Uhamiaji visiwani Zanzibar hii leo,
Waziri wa mambo ya ndani katika picha ya pamoja na maafisa wa juu wa idara ya Uhamiaji-Zanzibar.
Mh:Mwigulu Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na watumishiwa idara ya Vitambulisho vya Taifa-NIDA -Zanzibar.
Mwigulu Nchemba akizungumza na watumishi wa jeshi la polisi,NIDA na Uhamiaji katika Bwalo la polisi-Ziwani hii leo.
Katika
mengi aliyozungumza nao,Mh:Mwigulu amesisitiza kuongeza nguvu katika
mapambano dhidi ya biashara haramu ya madawa ya kulevya hasa katika
usafirishaji majini na maeneo wanayouzia madawa hayo.
Pia,Mwigulu
Nchemba ameweka bayana kuwa ni lazima jeshi la polisi lifanye kazi kwa
umoja wa hali ya juu ilikuhakikisha ulinzi na usalama unaendelea
kuimarisha nyakati zote.
Katika
hatua nyingine,Waziri wa mambo ya ndani ametoa fursa kwa watumishi wa
wa wizara anayoiongoza kutoa kero,changamoto au maoni ambayo yangetumika
kuboresha utendaji wa idara anazoiongeza.Katika kero kubwa ambazo
askari wameendelea kusisitiza ni makazi na maslahi na malimbikizo ya
madeni ya uhamisho na upandshaji wa vyeo kwa wakati.
Mmoja
wa afisa wa idara ya mambo ya ndani akichangia maoni yake na kero
zinazopaswa kurekebishwa ilikupambana na wahamiaji haramu katika mipaka
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mh:Turky
ambaye ni Mbunge wa moja ya jimbo kisiwani Unguja akitoa neno la
shukrani kwa waziri kwa namna alivyojitoa kuhakikisha anatatua kero za
askari na watumishi wote wa wizara ya mambo ya ndani.
Mwisho,Waziri
wa mambo ya ndani amekutana na askari wa jeshi la polisi waliostaafu
kwaajili ya kusikiliza ushauri wao katika kuimarisha utendaji kazi wa
idara za mambo ya ndani.
Pciha/Maelezo na Festo Sanga Jr.
No comments:
Post a Comment