Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa
maelekezo kwa Mkuu wa Kivuko cha MV. Chato, Eng. Fredinand Mishamo (Wa
kwanza kushoto), alipokagua kivuko hicho, wilayani Chato, mkoani Geita.
Fundi
wa Kivuko cha Mv Chato kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme Nchini
(TEMESA), Bw. Mbondo Jackson, akimweleza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, namna injini ya Kivuko cha MV.
Chato inavyotumia mafuta, alipotembelea kivuko hicho, wilayani Chato,
Geita.
Muonekano wa Kivuko cha MV Chato kilichopo Wilaya ya Chato mkoani Geita.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga, akimuonesha
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa
(mwenye shati la blue), ramani inayoonesha mtandao wa barabara za mkoa
wa Geita, alipomtembelea Ofisini kwake.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akisisitiza
jambo kwa wafanyakazi wanaofanya kazi kwenye Sekta ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano (hawapo pichani), alipoongea nao Mkoani Geita.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa,
akisalimiana na wafanyakazi wa Sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
mara baada ya kuongea nao Mkoani Geita.
Serikali
kupitia Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), imeanzisha Kitengo maalum
cha Wahandisi Washauri (TECU), ili kuwajengea uwezo wahandisi wazawa
kusimamia miradi ya ujenzi wa barabara nchini na hivyo kuokoa kiasi
kikubwa cha fedha ambacho kingetumika kuwalipa wahandisi washauri kutoka
nje ya nchi.
Akizungumza
mkoani Geita mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya
Uyovu-Bwanga-Biharamulo yenye urefu wa KM 112 ambayo pia inasimamiwa na
Wahandisi Washauri Wazawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Prof. Makame Mbarawa amesema mpaka sasa wahandisi wazawa wanasimamia
miradi mbalimbali ya barabara katika mikoa ya Kagera, Mwanza, Geita na
Kilimanjaro ambapo kupitia miradi hiyo serikali imeokoa dola za kimerani
milioni mbili ambazo zingetumika kulipa wahadisi kutoka nje ya nchi.
“Nitahakikisha
ninakijengea uwezo kitengo hiki ili kuweza kuokoa fedha nyingi zaidi.
Nimeridhishwa na usimamizi wa wahandisi hawa katika barabara hii ambayo
ipo katika hatua nzuri”, amesema Prof Mbarawa.
Waziri
Mbarawa ameongeza kuwa Serikali itahakikisha kuwa miaka mitano ijayo
miradi yote mikubwa nchini itasimamiwa na Wakala huo ili kuokoa fedha za
ndani na badala yake fedha hizo kuelekezwa kwenye miradi mingine ya
ujenzi.
Kwa
upande wake, Meneja wa TANROADS, mkoa wa Geita Eng. Harun Senkuku
amesema kuwa mradi wa ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga umefikia
asilimia 47 na Bwanga – Biharamulo umefikia asilimia 42 na ujenzi wake
unagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 90.
Aidha,
Eng. Senkuku amemuahidi Waziri huyo kukamilisha ujenzi huo kwa wakati
ili wananchi wa mikoa ya kagera na Geita kuweza kutumia barabara hiyo.
Naye,
Mhandisi Msahauri kutoka TECU Eng. Gladson Yohana amesema kuwa kusimamia
miradi mikubwa kama hiyo kumewasaidia kujifunza zaidi kwa vitendo na
amemuhakikishia Waziri huyo kusimamia barabara hiyo kwa kuzingatia ubora
na viwango vinavyotakiwa.
Katika
hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa amekagua kivuko cha MV. Chato na
kumuagiza Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), mkoa wa
Geita Eng. Fredinand Mishamo kuhakikisha kuwa kivuko hicho kinajiendesha
chenyewe kutoka kwenye mapato yanayopatikana.
Prof
Mbarawa amemtaka Meneja huyo kuhakikisha kuwa mapato yatokanayo na
kivuko hicho yanaongezeka ili kuweza kusaidia changamoto ndogondogo
katika kivuko hicho.
Eng.Mishamo amemuelezea Waziri huyo changamoto zinazokabili kivuko hicho kuwa ni kukosa maegesho katika baadhi ya maeneo.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilian
No comments:
Post a Comment