Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Lecri Consult, Legal and Child Right Consult,
Edna Kamaleki (kushoto), akizungumza na vijana wasomi katika warsha ya
siku moja ya kuwaongezea uwezo iliyofanyika Dar es Salaam leo. Warsha
hiyo iliandaliwa na taasisi hiyo.
Mdau Julius Kionambali (kushoto), akizungumza katika warsha hiyo.
Miriam Mnada (kulia), akichangia mada
Vijana wasomi wakiwa kwenye warsha hiyo.
Warsha ikiendelea.
Vijana wakisikiliza mada kwa makini
Na Dotto Mwaibale
VIJANA
wasomi wametakiwa kuacha kutegemea kazi za kuajiriwa badala yake wawe
wabunifu katika masuala mbalimbali kulingana na elimu yao ili kujikomboa
kiuchumi.
Mwito
huo umetoewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Lecri Consult, Edna
Kamaleki Dar es Salaam leo katika warsha ya siku mbili ya kuwaongezea
uwezo vijana iliyoandaliwa na taasisi hiyo.
"Kijana umesoma kwanini upoteze muda wako kwa kuzunguka kutafuta kazi wakati fursa nyingi zipo" alisema Kamaleki.Kamaleki
aliwataka vijana waoshiriki warsha hiyo kubadili na kuthubutu kuanza
kufanya kitu chochote kulingana na elimu walizosomea vijana hao.
Akizungumzia
taasisi yake hiyo alisema imejikita kutoa huduma za kisheria kwa jamii
na ushauri katika mambo mbalimbali yanayohusu haki za watoto."Tuna
amani kwamba haki za watoto ni muhimu kwa maendeleo na ustawi wa
watoto, pia watoto wanapaswa kuishi katika jamii ambayo haki za binadamu
na sheria zinaeleweka vizuri na kuheshimiwa na kila raia" alisema
Kamaleki.
Alisema
taasisi hiyo inatoa ushauri na huduma ya kisheria kwa jamii wakiwemo
watoto, watu binafsi na taasisi mbalimbali na kuandaa nyaraka
mbalimbali za kisheria na mikataba ya kisheria.
Aliongeza
kuwa shughuli zingine zinazofanywa na taasisi hiyo ni kushauri namna ya
kufungua kesi katika masuala ya jinai, madai, ndoa, ardhi na usimamizi
wa mirathi pamoja na kuwawakilisha wateja wao mahakamani katika shauri
lolote la kisheria.
Alitaja
kazi nyingine ya taasisi hiyo kuwa ni kuwasaidia watu binafsi kuunda na
kusajili kampuni au taasisi na kujenga uwezo wa taasisi au watu binafsi
kuhusu sheria mbalimbali za nchi na kimataifa na kufanya tafiti
mbalimbali kuhusu masuala ya kisheria.
Kwa
mawasiliano na taasisi hiyo wasiliana nao kwa facebook lecriconsult,
twitter lecriconsult na instrag ni lecriconsult1601 na simu namba
0767855174 na 0657023585.
No comments:
Post a Comment