Mbunge
wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla jioni hii ya
leo Oktoba 13.2016 amekaribishwa na dhehebu la Bohora na kuombewa dua
maalum na Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna Mufaddal
Saifuddin katika msikiti wa dhehebu hilo Upanga Jijini Dar es Salaam.
Mbali
na kutoa dua kwa Dk. Kigwangalla, Sheikh Dkt. Syedna ameahidi kuleta
wawekezaji wa Kibohora kutoka sehemu mbalimbali Duniani kwa ajili ya
kuwekeza kwenye ujenzi wa Mahospitali ikiwemo Hospitali za Rufaa za
kisasa pamoja na Viwanda vya Dawa hali ambayo itapunguza idadi ya
wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa ajili ya kufuata matibabu.
Pia viwanda vya dawa vitashusha gharama za dawa nchini na kupunguza ucheleweshaji unaosababishwa na kuagiza dawa nje ya nchi.
Aidha,
katika tukio hilo, usiku huu, Dk.Kigwangalla ameweza kushuhudia ndoa za
Vijana zaidi ya 50 zikifungishwa na Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani,
Dkt. Syedna.
Mbali
na Dk.Kigwangalla kuombewa dua maalum na Sheikh Mkuu wa Mabohora
Duniani, Dkt. Syedna, Mbunge wa Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa
Mambo ya ndani ya nchi, Mh. Mwigulu Nchemba aliungana katika kuombewa
na Shehe huyo.
Mbunge
wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa na
Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin (kulia)
wakati wa kuombewa dua maalum usiku huu.
Sheikh
Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin (kulia)
akimuombea Dua maalum Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla (kushoto aliyefumba macho)
Dua zikiendelea
Mbunge
wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akibusu mkono
wa Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin
isharara ya kupokea dua katika tukio hilo
Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin akimuaga Dk.Kigwangalla baada ya dua
Mbunge wa Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mh. Mwigulu Nchemba akiombewa dua katika tukio hilo.
Watu
kutoka Mataifa mbalimbali Duania ikiwemo jamii ya Bohora ambao pia
wapo hapa nchini nao wamepata bahati ya kuombewa dua maalum na Shehe
huyo Mkuu
Mbunge
wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoka
katika tukio hilo la kuombewa dua
Mbunge
wa Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mh.
Mwigulu Nchemba akitoka katika tukio hilo la kuombewa dua
Mbunge
wa Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mh.
Mwigulu Nchemba akisalimiana na Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh.
Dk. Hamisi Kigwangalla wakati wa tukio hilo
Picha ya pamoja
Mbunge
wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akipata picha
pamoja baadhi ya vijana ambao walipata kufunga ndoa na wake zao ndoa
ambazo zaidi ya 50 zimefungwa huku Shehe Mkuu huyo wa Mabohora Duniani
pia alipata kuzibariki.
No comments:
Post a Comment