Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli
Na Beatrice Lyimo-Maelezo
Na Beatrice Lyimo-Maelezo
9/12/2016
Dar es Salaam
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaendeleza jitihada zilizoachwa na Serikali za awamu zilizopita ili kuzidi kuwaletea maendeleo Watanzania.
Ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara yaliyofanyika katika uwanja wa uhuru Jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imeanza jitihada za kuboresha huduma za maendeleo ya jamii, ambapo katika bajeti ya mwaka 2016/17 imeamua kutenga asilimia 40 ya bajeti katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo umeme, miundombinu, afya, elimu.
“Mbali na kujiwekea vipaumbele mbalimbali kwa maendeleo ya nchi, kumekuwa na changamoto kadha wa kadha zinazozikabili nchi ikiwemo ufisadi, rushwa ndani ya baadhi ya watendaji” alisema Rais Magfuli.
Aidha Rais Magufuli alisema juhudi zinazoendelea kufanywa na Serikali ni kuboresha maslahi kwa watanzania kwa kuchukua hatua mbalimbali za kuwawajibisha wale wote wanaojihusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi.
Akifafanua zaidi Rais Magufuli aliwataka watanzania kudumisha amani na kulinda muungano uliyopo kwani amani ni msingi wa maendeleo ya nchi bila amani hakuna maendeleo.
Rais Magufuli pia alitoa wito kwa wantanzania kuendelea kufanya kazi kiwa bidii kwani kila mwananchi ana haki ya kufanya kazi, na kusema kuwa waasisi wa nchi walileta uhuru kwa maendeleo ya nchi kwani Uhuru ni kazi.
“Serikali ya Tanzania imejipanga kufanya kazi, tutafanya kazi kwelikweli, watendaji niliowachagua wanafanya kazi hivyo watanzania kwa ujumla mnatakiwa kuonesha ushirikiano kwao kwa maendeleo ya nchi yetu” alisema Rais Magufuli.
Mbali na hayo Rais Magufuli alisema kuwa ndani ya miaka 55 ya Uhuru Tanzania imepata mafanikio makubwa ambapo Tanzania imelinda Uhuru wa nchi, sambamba na kulinda mipaka iliyopo.
RAIS DK. MAGUFULI ASHIRIKI NA KUHUTUBIA KATIKA SHEREHE ZA MIAKA 55 YA UHURU WA TANZANIA BARA KATIKA UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi waliojitokeza katika sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi waliohudhuria sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama wakati wimbo wa Taifa ulipokuwa ukipigwa uwanjani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride katika sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Wanamaji kikipita mbele ya mgeni Rasmi kwa mwendo wa pole katika sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikipita mbele ya mgeni Rasmi kwa mwendo wa haraka katika sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Maadhimisho cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania kikionesha gwaride la kimyakimya mbele ya Amiri Jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Uhuru.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mama Fatma Karume mara baada ya kumaliza kuhutubia katika uwanja wa Uhuru.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi katika uwanja wa Uhuru mara baada ya kumalizika kwa sherehe hizo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembea pamoja na Askari Polisi ambao huongoza misafara ya viongozi VIP riders mara baada ya kuwasili Ikulu wakati wakitokea katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi mara baada ya Kuwasili katika uwanja wa Uhuru.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda mara baada ya kuwasili. (Picha zote na IKULU)

No comments:
Post a Comment