Tuesday, January 3, 2017

Wahamiaji wanavyojificha wakitaka kuingia Uhispania


Maafisa wa polisi wa Cueta walichapisha picha hii siku ya JumapiliImage copyrightGOOGLE
Image captionMaafisa wa polisi wa Cueta walichapisha picha hii siku ya Jumapili

Maafisa wa polisi wamewakamata raia wawili wa Morocco ambao walijaribu kuwaingiza wahamiaji katika eneo linalotawaliwa na Uhispania lililo kazkazini mwa Afrika la Cueta- wawili hao wakiwa wamejificha ndani ya gari na mwengine katika sanduku.
Wakati maafisa wa polisi walipokagua gari moja siku ya Jumatatu ,mtu mmoja alipatikana amefichwa katika eneo la mbele la gari na mwengine amefichwa katika eneo la kiti cha nyuma cha gari.
Mwanamume huyo na mwanamke ,wanaodaiwa kuwa raia wa Guinea ,walipata huduma ya kwanza kwa kuwa walikuwa na hewa kidogo ya kupumua.

Mtu mwengine alipatikana amefichwa katika eneo la gari la mbele maarufu dashboardImage copyrightEPA
Image captionMtu mwengine alipatikana amefichwa katika eneo la gari la mbele maarufu dashboard

Kwengineko kijana mmoja wa asili ya Kiafrika alipatikana amefichwa katika sanduku la mwanamke.
Kisa hicho kilitokea mnamo mwezi Disemba 30 na mtu huyo anayeaminika kutoka Gabon alihitaji matibabu ya dharura.
Mwanamke mwenye umri wa miaka 22 kutoka Morocco alijaribu kumuingiza Cueta, lakini maafisa wa uhamiaji walimuagiza kufungua sanduku lake ambalo lilikuwa limefungwa katika kitoroli.
Kisa hicho kinajari wakati ambapo kumekuwa na jaribio la wahamiaji wengi kuvunja ua wa mita sita unaogawanya Cueta na Morocco.

Mwengine alipatikana amefichwa chini ya kiti hiki kilichotengezwa ili kumtoshaImage copyrightGOOGLE
Image captionMwengine alipatikana amefichwa chini ya kiti hiki kilichotengezwa ili kumtosha

Raia 50 wa Morocco na 5 wa Uhispania walijeruhiwa wakati wahamiaji 1,100 walipojaribu kupita ua huo na kuingia Cueta kutoka Morocco.
Hakuna aliyefanikiwa kupita ,lakini watu wawili walijeruhiwa walipokuwa wakivunja ua huo na kupelekwa hospitalini huko Ceuta.
Mlinzi mmoja alipoteza jicho lake kulingana na maafisa.
Kisa kama hicho mnamo tarehe 9 Disemba kilihusisha zaidi ya wahamiaji 400 kutoka Afrika.

Ramani ya eneo la Cueta linalotawaliwa na Uhispania
Image captionRamani ya eneo la Cueta linalotawaliwa na Uhispania

Kumekuwa na majaribio kama hayo yanayofanywa na Waafrika wanaoishi kiharamu nchini Morocco, ambao hujaribu kuingia Ulaya.
Melila- nchini Uhispania pia ni eneo jingine linalolengwa na wahamiaji.

No comments:

Post a Comment