Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Diwani
wa Kata ya Mbagala Kuu Yusuf Manji amefika katika kituo cha kati
(Central Police) kwa ajili ya mahojino.Manji ambaye ni mwenyekiti wa
klabu ya Yanga aliwasili majira ya saa 5 asubuhi akiongozana na mawakili
wake.Baada ya kuwasili, Manji alisalimiana na wanachama wa klabu ua
Yanga na kuingia moja kwa moja kituoni kuendelea na taratibu nyingine.
Mwenyekiti
wa klabu ya Yanga ,Yusufu Manji akiwasili katika kituo cha Polisi Kati
jijini Dar es Salaam mara baada ya kuamua kujipeleka hapo yeye mwenyewe
kutii agizo la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda,ambaye watuhumiwa wote 65
aliowataja jana katika sakata la dawa za kulevya,aliwataka kufika kesho
Ijuma kituo cha Polisi kati kwa mahojiano zaidi.
Yusufu
Manji akipokelewa na baadhi ya wanachama wa Yanga katika kituo cha
Polisi kati mara baada ya kujipeleka leo badala ya kesho
Manji akisalimiana na wanachama wa Yanga katika kituo cha Polisi Kati
Mnaji akiwa akiwa ameongozana na mawakili wake na wasaidizi kuingia kituo cha kati jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Yanga Yusufu Manji akisalimiana na Waandishi wa Habari jijini Dar ess Salaam katika kituo cha Polisi Kati
No comments:
Post a Comment