KAIMU Mkuu wa Mkoa wa
Tanga, Mhandisi Mwanasha Tumbo ameziagiza wilaya zote za mkoa huu kuunda
majukwaa ya wanawake kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo ili yaweze kuwa chachu
ya kuwakomboa kimaendeleo na kiuchumi.
Mhandisi Mwanasha ambaye
pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza aliyasema hayo hivi karibuni wakati
akizindua jukwaa la wanawake mkoani Tanga ambalo litakuwa na malengo makuu ya
kuwainua na kuwawezesha wanawake kiiuchumi lililofanyika ukumbi wa ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Alisema
uwepo wa majukwaa hayo itasaidia kutoa fursa kwa wanawake kuweza kushiriki
kikamilifu kwenye masuala mbalimbali ikiwemo kuwepo na majukumu ya kuwawezesha
wanawake kuweza kujiinua kiuchumi kutokana na shughuli wanazozifanya zikiwemo
za ujasiriamali.
Aidha
pia aliwataka wanawake kuwa mstari wa mbele kuzalisha bidhaa bora na wenye
kiwango cha kimataifa ili waweze kupata nafasi ya kuziuza ndani na nje ya nchi
ili kuwasaidia kuongeza pato lao na Taifa kwa ujumla.
“Wajasariamali
warasimishe biashara zao ili ziweze kutambulika
kisheria
ikiwemo kulipa kodi lakini pia muachane na suala la
kujiingiza
kwenye biashara haramu ambazo zinaweza kukatisha ndoto zenu “Alisema.
“Kupitia
Jukwaa hili mnaweza mnalitumia kusaidia wanawake kujikwamua kiuchumi na kuweza
kufia sera ya asilimia 50 kwa 50 hivyo ili kufikia huko jukumu lenu kuonyesha
uwezo lakini pia wekezeni kwenye elimu kupitia mkusanyiko huu “Alisema.
Awali
akizungumza Mjasiriamali wa kampuni ya kutengeneza Fenicha, za majumbani na
maofisini mkoani Tanga Edna Boimanda aliwashauri wanawake kuunganisha nguvu za
pamoja ili kuona namna ya kuanzisha benki ya wanawake kwani hiyo ndio fursa ya
kipekee wanayoweza kujikwamua kiuchumi.
Alisema
kupitia benki hiyo itawawezesha waanawake kujiletea maendeleo kwa kupata mikopo
itakayokuwa chachu ya kufikia malengo yao ya kupata mafanikio.
Mmmoja
wa Wajasiriamali kushoto akimuonyesha Kaimu Mkuu wa Mkoa wa
Tangaa,Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza
akiangalia moja kati ya bidhaa wanazozalisha wakati wa kongamano la
wanawake wajasiriamali mkoani Tanga lililofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga hivi karibuni.
Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto aliyevaa hijabu
ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza akipata maelekezo kutoka kwa
mmoja wa wanawake wajasiriamali wakati alipofungua jukwaa la wanawake
mkoani Tanga hivi karibuni.
Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye pia ni Mkuu wa
wilaya ya Muheza kulia akipata maelekezo kutoka kwa mmoja wa wanawake
wajasiriamali wakati alipofungua jukwaa la wanawake mkoani Tanga hivi
karibuni.
Picha na habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
No comments:
Post a Comment