Wednesday, June 7, 2017

Adnan Khashoggi: Tajiri Msaudia afariki London akiwa na miaka 82

Adnan Khashoggi and his wife LamiaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionAdnan Khashoggi na mkewe Lamia mwaka 2005
Mfanyabiashara wa silaha Adnan Khashoghi ambaye ni tajiri anayefahamika kwa maisha yake ya kifahari amefariki mjini London akiwa na umri wa miaka 82.
Familia yake kwenye taarifa ilisema kuwa alifariki akiwapata matibabu ya maradhi ya kutetemeka.
Bwana Khashoggi alikuwa mmoja kati ya watu matajiri zaidi duniani miaka ya 1970 na 80 kwa kupata kandarasi za kimataifa za kuuza silaha.
Karamua zake zilikuwa za aina yake ambazo mara nyingi zilichukua siku kadha.
Bwana Khashoggi aliiwakilisha ufaransa katika mbioa dhidi ya Uingereza ya kushinda kandarasi ya dola bilioni 20 kuiuzia Saudi ASrabia silaha, kandarasi iliyopo hadi sasa.
Donald Trump bought Khashoggi's NabilaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionDonald Trump aliinunua Nabila na kuipa jina Trump Princess
Alitumikia kifungo gerezani nchini Uswisi miaka ya 1980 na kupinga kusafirishwa hadi nchini Marekani baada ya madai ya kumsaidia aliyekuwa rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos kuficha pesa.
Wakati mmoja bwana Khashoggi alikuwa mmiliki wa mashua kubwa zaidi duniani Nabila, ambayo ilitumiwa katika filamu ya James Bond ya Never Say Never Again.
Wakati biashara yake ilikumbwa na matatizo ya kifedha aliisalimisha mashua huyo kwa Sultan wa Burunei ambaye aliiuza kwa Donald Trump ambaye sasa ni rais wa Marekani kwa kima cha dola 29,000 miaka ya 1980.
Mfanyabiashara huyo ambaye dadake Samira alikuwa mke wa tajiri Mohammed Al Fayed pia alikuwa mjomba wa mpenzi wa Princess Diana Dodi Fayed.

No comments:

Post a Comment