Wednesday, June 7, 2017

Theresa May kubadili sheria ya kupambana na ugaidi

Uingereza
Image captionWaziri mkuu wa Uingereza, Theresa May
Waziri mkuu wa Uingereza, Theresa May, amesema yuko tayari kubadilisha sheria yoyote ya haki za binadamu ambayo inazuia polisi na vikosi vya usalama kupambana ipasavyo na tishio la ugaidi.
Wahusika katika chama chake cha Conservative wameashiria kwamba iwapo waziri mkuu May atachaguliwa tena, serikali yake itakuwa tayari kujitoa katika sheria za jumuia ya ulaya za kutetea haki za binadamu.
Katika moja wapo ya hotuba zake za mwisho za kampeni, May amesema anataka kurahisisha kuzuia uhuru wa magaidi na kuwarudisha katika nchi zao za asili.
Kauli yake hiyo inafuatia shambulio la hivi majuzi lililofanyika jijini London na kuuwa watu kadhaa.
Wakati huo huo, waziri wa mambo ya nje wa Australian, Julie Bishop, amethibitisha kwamba raia wa pili kutoka Australia ni miongoni mwa watu saba waliouawa katika shambulio la Jumamosi.
Vyombo vya habari vya nchi hiyo vinasema raia huyo ni Sara Zelenak, ambae waziri mkuu amesema siku ya Jumanne kwamba ana wasi wasi.
Raia wawili wa ufaransa na mmoja kutoka Canada pia inaamika kuwa miongoni mwa waliouawa.
Mjomba wa mmoja kati ya washambuliaji mwenye asili ya Pakistani ameiambia BBC kwamba analaani shambulio hilo na kwamba yuko pamoja na wanaoomboleza mauaji hayo.

No comments:

Post a Comment