Wednesday, June 7, 2017

Trump aisifu Saudi Arabia kwa kuitenga Qatar

MarekaniHaki miliki ya pichaAP
Image captionRais wa Marekani Donald Trump
Rais Trump ameungana na nchi ya Saudi Arabia katika mgogoro wa kidiplomasia unaoendelea na Qatar, huku akiusifu msimamo wa nchi hiyo ya tawala ya kifalme wa kuitenga nchi jirani baada ya Qatar kutuhumiwa kusaidia kifedha makundi yenye msimamo mkali.
Trump ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba hatua hiyo inaweza kuwa ndio mwanzo wa kutokomeza tishio la ugaidi.Katika mkutano na waandishi wa habari, msemaji wa ikulu ya Marekani, Sean Spicer, amesema mgogoro huo umekuwa ukifukuta kwa muda mrefu.
"kumekuwa na wasiwasi wa muda miongoni mwa nchi jirani na Qatar. Marekani inaendelea kuwasiliana kwa karibu na nchi zote ili kutatua mgogoro unaoendelea na kurudisha hali ya ushirikiano ambayo ni muhimu kwa usalama wa eneo.
Nadhani, katika ujumbe wake, kuna hali ya kutilia mkazo suala la kudhamini ugaidi unaofanywa na baadhi ya nchi katika eneo hilo, lakini Marekani bado inataka huu mdororo wa uhusiano wa kidiplomasia utatuliwe haraka iwezekanavyo."Bwana Spicer amesema kwamba kiongozi wa Qatar yuko katika mapambano dhidi ya ugaidi.
"Rais amefanya mazungumzo yenye tija kabisa na kiongozi wa Qatar pindi alipokuwa katika ziara yake huko mjini Riyadh. Wakati huo, aliguswa sana na azma ya kiongozi huyo ya kutaka kujiunga rasmi katika kudhamini kituo cha kupambana na ugaidi na kuonyesha ari yao katika suala hilo."Waziri wa mambo ya nje wa Qatari ametaka kuwepo na majadiliano ya wazi kuhusu tuhuma hizo.
"Tumefanya mkutano wa moja kwa moja wa tais Trump, baina yake na Amir na ametuambia wazi wazi kwamba ameona kuna tuhuma kwa baadhi ya nchi katika eneo hilo kwamba zinadhamini ugaidi, na amerudia kauli hiyo mara kadhaa. Tumemwambia wazi kwamba iwapo anaona kuna tuhuma zozote, basi tunaweza kukaa mezani na kuzitatua.Waziri huyo wa Qatar ameendelea kusema kuwa hakuna ushahidi wowote unaoonyesha kwamba Qatar imejihusisha katika kudhamini magaidi:"
Jamii ya kiitelijensia na uhusiano wa serikali kwa serikali, wote wanajua kuhusu uhusiano baina ya Qatar ushirikiano baina ya Qatar na Marekani. Hakuna ushahidi hata mmoja unaonyesha serikali ya Qatar kuunga mkono makundi ya waislamu wenye siasa kali.")
Wakati huo huo, nchi kadhaa ikiwemo Uturuki, zimeonyesha wasiwasi wake kutokana na kuzorota kwa uhusiano katika eneo hilo la Gulf.
Rais wa Uturuki amejitolea kupatanisha mgogoro huo huku akisema kutengwa na vikwazo havitatatua mgogoro huo.
Lakini Jordan nayo imesema itapunguza uwakilishi wake wa kidiplomasia na Qatar na kufuta leseni ya kituo cha televisheni ya Al Jazeera. Kiongozi wa Kuwait anaelekea nchini Saudi Arabia kujaribu kutatua mgogoro huo.

No comments:

Post a Comment