Saturday, July 21, 2012

Je hii taarifa inamanufaa gani kwa sasa na kwanini hatua za kisheria hazikuchuliwa kama kuna ukweli kuhusu boti ya skagit

Skagit ilishindikana kutumika Marekani

Meli Yenyewe ikiendelea kuzama
Taarifa zinaonyesha kwamba boti ya Skagit ni kati ya zilizonunuliwa nchini Marekani mapema mwaka jana baada ya kuonekana haifai kwa matumizi nchini humo.

Ripoti za vyombo vya habari vya Marekani zinaonyesha kwamba boti hiyo ni kati ya mbili zilizonunuliwa Februari mwaka jana baada ya kutofanya kazi tangu Septemba mwaka 2009, ikiwa ni utekelezaji wa wabunge kushinikiza zisitumike kwa usafirishaji wa abiria tangu mwaka 2006.

Awali, boti hizo ambazo ni Kalama na Skagit, zilikuwa zinamilikiwa na serikali ya jimbo la Washington ambayo iliziuza kwa kampuni ya ununuzi wa boti Port Coquitlam, B.C, ambayo baadaye iliziuza Tanzania.

Taarifa zinaeleza kuwa zote mbili ziliuzwa kwa bei ya kutupa ya dola za Marekani 400,000 tofauti na thamani yake iliyokuwa imeelezwa Desemba mwaka 2009 ya dola za Marekani 900,000.

Gazeti la Times la Februari 18, mwaka jana lilimkariri msemaji wa Feri Jimbo la Washington, Marta Coursey, akieleza kuwa meli hizo zingesafirishwa na meli ya mizigo kwenda Afrika, Tanzania.

Gazeti hilo lilieleza kuwa uuzaji wa boti hizo ulifanyika ikiwa ni mpango wa serikali ya jimbo la Washngton kuziua nchini humo, ambao hata hivyo ulishindikana.



Baadaye ililazimu kuziingiza kwenye mnada wa mtandao ikitaka kuziuza kwa dola za Marekani 300,000 kwa kila moja lakini pia haikufanikiwa na badala yake ziliuzwa kwa dola za Marekani 400,000 mwaka jana.

Zilitengenezwa New Orleans na zilinunuliwa mwaka 1989 kwa dola za Marekani milioni tano.

Mwanahistoria wa Feri jimboni humo, Steve Pickens, alikaririwa na gazeti la Times kwamba boti Kalama na Skagit, zilikuwa ni za kwanza za abiria zilizotengenezwa na serikali.

Baada ya tetemeko la ardhi la Loma Prieta, mwaka 1989, boti zote mbili zilitumwa San Francisco na kusaidia usafiri wakati ujenzi wa madaraja ya mji huo yakijengwa.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment