Friday, November 8, 2013

Makubaliano na Iran kuhusu Nuklia yanukia

 

Maungumzo kuhusu mpango wa Nuklia wa Iran mjini Geneva
 
Waziri wa mambo ya nje wa Iran, amesema kuwa anaamini makubaliano kuhusu mpango wake wa Nuklia yataafikiwa mwishoni mwa Ijumaa.
 
Mohammad Zarif ameambia CNN kuwa Iran haitasitisha mpango wake wa kurutubisha madini ya Uranium kabisa lakini inaweza kujizuia naa baadhi ya maswala yanayozungumziwa.
 
Nchi za magharibi hata hivyo hazikuzungumzia hatua iliyofikiwa katika mazungumzo hayo mjini Geneva.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, ambaye anazuru Mashariki ya Kati, anatarajiwa kuhudhuria mazungumzo hayo siku ya Ijumaa.

Mwandishi wa BBC aliye kwenye msafara wa Bwana Kerry, anasema kuwa uamuzi wake kubadili mipango yake ya safari nchini Saudi Arabia na kwenda Geneva, ni dalili tosha kuwa mkataba huenda ukaafikiwa kati na Iran

Mnamo siku ya Alhamisi, Marekani ilithibitisha kuwa baadhi ya vikwazo dhidi ya Iran vitalegezwa ikiwa Iran itachukua hatua muhimu na ambazo zinaweza kuthibitishwa katika mpango wake wa nuklia.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, amesema kuwa ikiwa mkataba utafikiwa litakuwa kosa la kihistoria na kuituhumu Iran kwa kutokuwa mkweli.

Wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ikiwemo Ujerumani , walikutana kwa mazungumzo kuhusu Iran siku ya Alhamisi mjini Geneva.

Nchi za Magharibi zinashuku kuwa mpango wa Iran wa kurutubisha madini ya Uranium ni hatua ya kutaka kujenga zana za nuklia.

No comments:

Post a Comment