Sunday, August 24, 2014

Wachezaji wa Real Madrid Legend wawahenyesha wa Tanzania Eleven

*Wawapiga mabao 3-1
*Mamia wamiminika kuwashuhudia Uwanja wa Taifa
*Waifurahia safari yao ya Tanzania
*Reuben De la Red aifungia mabao 3 timu yake
*Akabidhiwa mpira wake na Rais Jakaya Kikwete
Baadhi ya mashabiki waliomiminika Uwanja wa Taifa, kushuhudia mpambano kati ya wachezaji wa zamani wa Real Madrid (Real Madrid Legend) na wazamani wa Tanzania (Tanzania Eleven), ni hii familia ya Fuad Edha Awadh, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mikoani Traders, wamiliki wa viwanda vya Azania vinavyosaga na kusafirisha nafaka za aina mbalimbali nchini na nje ya nchi na wazalishaji wakubwa wa unga wa ngano wa Azania wheat flour. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mashabiki wakisubiri mchezo kuanza, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.
Timu zikiingia Uwanjani tayari kwa kuanza mchezo kati yao, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji wa timu zote mbili, wakiingia uwanjani tayari kwa mchezo huo wa kirafiki wa Kimataifa.
Timu ya Real Madrid Legend, ikisubiri kukaguliwa.
Timu ya Tanzania Eleven, ikisubiri kukaguliwa.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangala, akikagua timu, hapa akiikagua timu ya Real Madrid Legend.
Hapa wachezaji wa Real Madrid Legend, wakisalimiana na wa Tanzania Eleven kabla ya kuanza mchezo.
Wachezaji wa Real Madri Legend wakipiga picha ya kumbukumbu kabla ya kuanza mchezo huo.
Wachezaji wa Tanzania Eleven, wakipiga picha ya kumbukumbu kabla ya kuanza mchezo huo.
Rais Jakaya Kikwete, akielezwa jambo na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamali Malinzi. Kushoto ni Balozi wa Hispania nchini.
Wachezaji wa Real Madrid Legend na wa Tanzania Eleven, wakipiga picha ya pamoja kwa ajili ya kumbukumbu kabla ya mchezo.
Makapteni wa timu zote mbili, Mohammed Mwameja (kushoto) wa Tanzania na Andres Sabido wa Real Madrid Legend (kulia), wakipiga kura kuchagua goli la kuanzia.
Kikosi cha kilichoanza mchezo cha Tanzania Eleven, kikipiga picha ya kumbukumbu kabla ya kuanza mchezo.
Salum Sued wa Tanzania Eleven (kulia), akipiga mpira huku akifuatwa na Luis Figo wa Real Madrid Legend.
Luis Figo wa Real Madrid Legend, akikimbia na mpira katika kumtoka beki wa Tanzania Eleven, Shadrack Nsajigwa.
Mashabiki waliokuwa jukwaa kubwa, wakiangalia mchezo kati ya timu hizo za Real Madrid Legend na Tanzania Eleven, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni. 
Luis Figo wa Real Madrid Legend na beki wa Tanzania Eleven, Shadrack Nsajigwa, wakiwania mpira uliokuwa katikati yao.
Shaaban Ramadhan (kushoto), akijaribu kutaka kumzuia Ruben De la Red (kulia), wakati wa mchezo huo.
Mashabiki wakifuatilia mchezo kati ya timu hizo.


Wachezaji wa Real Madrid Legend wakishangilia goli lao la kwanza lililofungwa na Ruben De la Red (9), katika mchezo huo.
Luis Figo (kulia), akimpiga chenga beki Shaaban Ramadhani.
Shaana Ramadhan, akimdondosha Luis Figo katika kujaribu kumdhibiti.
Ruben De la Red, akimtoka beki Shadrack Nsajigwa.
Beki wa Tanzania Eleven, Shadrack Nsajigwa, akijaribu kumdhibiti Ruben De la Red wa Real Mdrid Legend. 
Christian Karembeu, akijaribu kuudhibiti mpira. 
Luis Figo, akimtoka Shadrack Nsajigwa.
Luis Figo na Shadrack Nsajigwa, wakiwania mpira wa juu.
Shadrack Nsajigwa, akijaribu kuudhibiti mpira uliokuwa ukiwaniwa na Luis Figo.
Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi mpira Ruben De la Red baada ya kuifungia timu yake mabao 3 katika mchezo huo.
Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi kombe Nahodha wa timu ya Real Madrid Legend, Andres Sabido, baada ya timu hiyo, kuifunga Tanzania Eleven mabao 3-1 katika mchezo huo.
Rais Jakaya Kikwete (katikati), akipiga picha ya kumbukumbu na wachezaji wa timu ya Tanzania Eleven baada ya kumalizika kwa mchezo baina ya timu hizo, ambapo Tanzania Eleven ilikubali kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Real Madrid Legend.
Rais Jakaya Kikwete (katikati), akipiga picha ya kumbukumbu na wachezaji wa timu ya Real Madrid Legend, baada ya kumalizika kwa mchezo baina ya timu hizo, ambapo timu hiyo, iliihenyesha Tanzania Eleven kwa kichapo cha mabao 3-1.
Ruben De la Red wa Real Madrid Legend, akiwa na kombe walilokabidhiwa na Rais Kikwete, mbele ya mashabiki waliokuwa wakiishangilia timu hiyo katika mchezo huo.

No comments:

Post a Comment