Mshambuliaji wa kujitoa muhanga amejipenyeza katika
mazowezi ya gwaride katika mji mkuu wa Yemen , Sanaa
leo na kuuwa watu 63 katika shambulio baya kabisa
dhidi ya mji huo katika miaka ya hivi karibuni ya nchi hiyo
kutokuwa na hali ya usalama.
Watu kadha , wengi wao wakiwa wanajeshi, pia wamejeruhiwa katika shambulio hilo, ambapo damu na sehemu za miili ya watu ilisambaa katika eneo kubwa.
Waziri wa ulinzi wa Yemen na mkuu wa jeshi pia walikuwapo wakati wa tukio hilo, la mazowezi ya gwaride kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya taifa hapo kesho Jumanne,lakini hawakujeruhiwa.
Maafisa wanatuhumu kuwa shambulio hilo limefanywa na mwanajeshi ambaye ni mkorofi. Mtu mmoja ambaye anadai kuwa anazungumza kwa niaba ya kundi la wapiganaji wa Ansar al-Sharia amesema kwa njia ya simu kuwa kundi hilo linahusika na shambulio hilo.

No comments:
Post a Comment