Tuesday, May 22, 2012

Viongozi wataka kumaliza vita vya Afghanistan

Viongozi  wa NATO wanaokutana  mjini  Chicago nchini Marekani  wanatathmini  upya  jukumu  lao  katika kumaliza vita  ambavyo  haviungwi  tena  mkono nchini Afghanistan  katika  mwaka  2014 na  kujitayarisha  kwa ajili  ya hatua nyingine  muhimu  mwakani, wakati majeshi ya  Afghanistan yatakapochukua uongozi  wa usalama wakati majeshi  ya kimataifa  yatachukua  jukumu la usaidizi.

 Hadi  sasa  mkutano  huo  wa  siku mbili  wa NATO , viongozi  wameeleza matumaini  yao  kuwa muongo mmoja  wa vita nchini  Afghanistan  unatoa nafasi kwa  muongo  wa  hatua  za  mpito  kuelekea  amani  na uthabiti, ukiongozwa  na  Marekani  na  washirika  wake.


 Baadhi  ya  mataifa  wanachama  wa  mfungamano  wa NATO , hivi  karibuni , Ufaransa , zimetaka  kuondoa majeshi  yao  mapema  kutoka  Afghanistan. Kundi  la wapiganaji  wa  Taliban  pamoja  na  washirika  wao limeonya  kuwa  wanasubiri  kujaza pengo nchini Afghanistan baada ya majeshi  ya  NATO  kuondoka.    

No comments:

Post a Comment