Tuesday, May 22, 2012

Zimbabwe yakana kuhusika na ghasia

Waziri  wa  sheria  wa  Zimbabwe  amekana  madai  kuwa nchi  yake  inaunga  mkono  kundi  linalofanya  ghasia nchini  humo  na  kuapa  kutotambua   haki  za mashoga baada  ya   kukutana  na  mkuu  wa  umoja  wa  mataifa wa  haki  za  binadamu.

Patrick  Chinamasa amesema kuwa  amemwambia  kamishna  wa  umoja  wa  mataifa  wa haki  za  binadamu Navy Pillay  kuwa  Zimbabwe itawakamata  watu  wanaohusiana  kimapenzi  wa  jinsia moja  wakikamatwa  wakifanya  vitendo  vya  ushoga.

 Pillay amewasili  jana  nchini  Zimbabwe  kwa  ajili  ya  ziara  ya wiki  moja, ikiwa  ni  ya  kwanza  kufanywa  na  taasisi  hiyo ya  kimataifa  nchini  humo

katika  azma  ya  kutathmini ukiukaji  wa  haki  za  binadamu. Chinamasa  amesema kuwa  Pillay  amealikwa   na  serikali  ya  mseto  nchini humo  iliyoundwa  mwaka  2009  baada  ya  uchaguzi uliobishaniwa  na  kusababisha  ghasia  ambazo ziliambatana  na  ukandamizaji  ambao  wanamgambo  wa chama  cha  rais  Robert  Mugabe  walilaumiwa  pamoja  na polisi  wanaounga  mkono  serikali  pamoja  na  jeshi.       

No comments:

Post a Comment