Matumizi ya simu za mkononi yamerahisisha mambo mengi barani
Afrika. Takriban kila mtu wa pili barani humo anasimu ya mkononi na
idadi inaongezeka kwa kasi.
Kwa mfano, katika robo ya eneo la kusini mwa jangwa la Sahara barani humo, watu wanaweza kuwasiliana kwa kupigiana simu, kuandikiana ujumbe wa SMS na mengine mengi. Bara la Afrika limo katika harakati za kuwa karibu na teknolojia mpya .
Mafanikio yake:
Nchini Kenya mfano kuna utaratibu wa kutuma fedha hata katika maeneo ya mbali nchini humo kwa kutumia simu ya mkononi. Utaratibu huo unajulikana kama M-Pesa na hata mkulima anaweza kufanya biashara ya mazao yake kwa kutumia utaratibu huo .
Kwa hiyo simu ya mkononi imekuwa chachu ya utandawazi katika bara la Afrika na kila mwaka kunapigwa hatua mpya.Katika mwaka 2005 kulikuwa na simu milioni 90 za mkononi barani humo na mwaka jana zikafikia karibu 450 milioni .
Wafanyabiashara wa Kichina wanamiliki soko zaidi kwa simu za rahisi, huku wafanyabiashara wa simu kutoka Ulaya nao wakiingiza mamilioni ya simu za kisasa katika soko la Afrika.
Mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa maendeleo, Joachim von Braun, anasema, katika uchunguzi uliofanywa miaka 10 iliopita ilionekana kwamba wakati huo kama kwamba simu ya mkononi haikuwa muhimu kwa binaadamu aliyeko sehemu za ndani barani humo, na badala yake muhimu yakihitajika maji na chakula. Lakini sasa wakati umebadilika na hata wale walio masikini katika nchi za kiafrika wamenufaika mno na chombo hicho- simu ya mkononi.
Ongezeko la matumizi :
Simu inarahisisha hata biashara
Mtafiti wa maendeleo von Braun anasema pia kumeanza hatua nyengine
katika maendeleo ya teknolojia katika bara la Afrika. Nayo ni ile ya
matumizi ya Internet. Umuhimu wake kwa nchi za kusini unaanza kuwa sawa na ule katika nchi zilizoendelea za kaskazini. Takwimu zinaonyesjha kwamba katika kila watu 100 , 12 wanatumia mtandao wa Internet .
Hata hivyo, mtaalamu wa maendeleo, Bern Friedrich, kutoka Shirika la ushirikiano wa maendeleo ya kimataifa, (GIZ), anasema bado ni miongoni mwa wakaazi wa mijini, wale ambao bila shaka wana fedha zaidi, na hasa wanaume kuliko wanawake, na bila shaka ni kwa vijana zaidi.
Ukuaji uchumi na matumizi ya simu za mkononi na Internet :
Kwa upande mwengine, kwa mujibu wa uchambuzi wa ukuaji uchumi uliofanywa na Benki ya Dunia 2009 ni kwamba katika nchi zinazoendelea ambako kuna uwezekano wa kutumia mtandao wa Internet, imeonekana kwamba ukuaji uchumi uliweza kufikia 1,4 asili mia kwa mwaka.
Hadi miaka iliopita, kulikuwa na watu takriban 5 tu katika kila 100 ambao walimudu kuwa na kadi ya ya matumizi ya Internet. Leo hii kuna mabadiliko makubwa na ongezeko limefikia karibu asili mia 160.
Afrika na kuimarishwa sekta ya mawasiliano:
Kuna matumaini ya kupunguwa kwa gharama za simu za mkononi na Internet barani Afrika , wakati nyaya za mawasiliano zinazopita baharini kutoka Marekani na Ulaya zitakapoongezeka kwenye mwambao wa pwani barani Afrika.
Matokeo yake yatakuwa ni kuimarika zaidi kwa teknolojia hiyo na matumizi yake katika bara hilo, iwe ni mjini Windhoek au Nairobi. Mfano mmoja wapo wa mafanikio ni Rwanda . Afrika kwa maneno mengine inazidi kuwa ni sehemu ya Ulimwengu wa teknolojia ya Digital.
No comments:
Post a Comment