WATU
13 akiwamo mjamzito wamefariki dunia, huku wengine 16 wakijeruhiwa
kufuatia ajali iliyotokea Mbeya mjini baada ya basi dogo aina ya Coaster
na lori aina ya Scania kugongana uso kwa uso.
Ajali hiyo ilitokea
jana saa 6:30 mchana eneo la Mlima Mzalendo, Igawilo baada ya basi hilo
lililokuwa limejaza abiria kutoka Mbeya kwenda Kyela liligongana na
lori lililokuwa na tela likitokea nchini Malawi.
Mashuhuda wa
tukio hilo walisema chanzo cha ajali hiyo ni breki za lori lililokuwa
likiteremka kushindwa kufanya kazi na kuvamia basi hilo kwenye kona kali
na kusababisha vifo hivyo.
Kwa mujibu wa maofisa wa polisi waliokuwa kwenye tukio hilo, watu waliokufa ni 13 na wengine 16 walijeruhiwa.
Walisema waliokufa papo hapo ni tisa na wanne walifia hospitalini wakiendelea kupata matibabu.
Miongoni
mwa waliokufa yumo dereva wa basi aliyetambulika kwa jina la Mwasa
Diamond (32), mkazi wa Ilomba, Mbeya na mwanamke mmoja aliyetajwa kuwa
alikuwa ni mjamzito ambaye hakufahamika jina lake.
Mkurugenzi wa
Hospitali ya Rufani Mbeya, Eliuter Samky, alithibitisha kupokea miili ya
marehemu na kwamba, hali za majeruhi zilikuwa mbaya.
Alisema
baadhi ya miili ya marehemu haijatambuliwa na amewataka wananchi
kujitokeza.Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Athuman Diwani, hakupatikana
kuzungumzia tukio hilo. |
No comments:
Post a Comment