KAMISHNA
Msaidizi wa Madini Kanda ya Kaskazini Mhandisi Benjamin Mchwampaka
amesema kuwa tatizo la ajira kwa watoto kwenye migodi ya Tanzanite
katika Mji Mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro limekomeshwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari juzi, Mchwampaka alisema ajira hizo zimekomeshwa
kutokana na juhudi za Wizara ya Nishati na Madini, wamiliki wa migodi
na jamii katika kuizuia wachimbaji wadogo.
“Nashukuru hivi sasa kwenye migodi ya Tanzanite hakuna kabisa wachimbaji
wanaowatumia watoto kuchimba madini, hivyo wameweza kuitikia katazo la
kutokuwatumia 'manyoka' kuchimba madini,” alisema Mchwampaka.
Alisema kitendo cha kuwatumikisha watoto kwenye machimbo ya madini
kilikuwa kikitoa picha mbaya na sifa isiyofaa duniani akishukuru kwamba
kwa sasa hakuna tena watoto wanaofanya kazi migodini.
Hata hivyo, asasi isiyo ya Serikali ya Good Hope Programme ya Mji mdogo wa Mirerani kupitia Mkurugenzi wake,Dorah Mushi imetajwa kutoa mchango mkubwa katika kupiga vita ajira mbaya ya watoto waliokuwa wakitumikishwa migodini.
Mushi aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Manyara (CCM)mwaka 2005-2010 alishiriki kikamilifu kutokomeza ajira hiyo.
Mikoa
ya Kanda ya Kaskazini ya Manyara, Arusha,Tanga na Kilimanjaro ilikumbwa
na tatizo la ajira kwa watoto ambao waliacha shule na kukimbilia
kufanya kazi katika migodi ya Tanzanite. |
|
No comments:
Post a Comment