SERIKALI
imetangaza mabadiliko ya Sheria mbalimbali zinazohusu kudi,
zitakazoathiri bei za bidhaa muhimu nchini kwa lengo la kuongeza mapato
ya Serikali.
Akisoma Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka
2012/13, Dk Mgimwa alisema kodi za bia, vinywaji baridi na vinywaji
vikali zitapanda kuanzia Julai Mosi mwaka huu.
Katika ongezeko
hilo, soda zitapanda kwa Sh14 kwa lita kutoka Sh69 hadi Sh83, bia yenye
kimea pekee itaongezeka kwa Sh62 kutoka Sh248 hadi Sh310 kwa lita wakati
bia nyingine zitaongezeka kutoka Sh420 hadi Sh525 kwa lita, sawa na
ongezeko la Sh105.
Vilevile kodi ya mvinyo unaotengenezwa kwa
zabibu zinazolimwa ndani imeongezeka kwa asilimia 75 kutoka Sh145 hadi
Sh420, sawa na ongezeko la Sh275 kwa lita.
Kuhusu mvinyo
unaotokana na zabibu za nje umeongezwa kodi kutoka Sh1,345 kwa lita hadi
Sh1,614 sawa na ongezeko la Sh269 kwa lita.
Vinywaji vikali vimeongezwa kutoka Sh1993 kwa lita hadi Sh2,393 sawa na ongezeko la Sh399. Bidhaa
nyingine iliyoongezwa kodi ni sigara za aina zote, ambazo zile zisizo
na kichungi zinazotumia tumbaku ya hapa nchini, imepanda kutoka Sh2,820
hadi 8,210 kwa sigara 1,000.
Wakati zile zenye kichungi na
tumbaku ya ndani zimeongezwa kutoka Sh16,114 hadi 19,410 kwa bunda;
wakazi zile nyingine zikipanda kutoka Sh29,264 hadi Sh35,117 kwa bunda.
|
|
No comments:
Post a Comment